TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 21 Novemba 2017

22:26

SAADA NASSOR AMTABILIA MAFANIKIO MAKUBWA KHADIJA MBEGU!.

Na pambe za taarab.

Muimbaji bora tanzania visiwani ambae mpaka sasa anaendelea kushikilia zile tuzo tatu za ubora wa uimbaji wa muziki huu wa taarab Saada nassor amemsifia na kumpongeza muimbaji chipukizi khadija mbegu kwa uimbaji wake baada ya kukutana nae katika show ya bendi ya gusagusa ijumaa na jumamosi pale Hugo house kinondoni jijini dar.

Unajua nilipomuona msichana huyu akiimba pale katika steji ya gusagusa nilivutiwa nae sana maana ananikumbusha mimi nilipokuwa naanza kuimba nilikuwa kama yeye...nilikuwa ni mwenye kipaji kikubwa kama yeye, nilikuwa na mwili mdogo kama wake, kiukweli anaimba vizuri sana! ana kipaji kikubwa sana ambacho kinatakiwa kuendelezwa na viongozi wake na pia juhudi zake binafsi zinahitajika.  Atakutana na vikwazo vingi sana, atavunjwa moyo, atakatishwa tamaa, atanyanyasika lakini ajue hayo yote yatamkuta kwakuwa hao wabaya wake wamegundua kuwa ana kipaji na muda wowote anaweza kuwazidi.

Mimi nimepitia katika mazingira magumu sana mpaka leo hii watu wananifahamu na napata mialiko kadhaa wa kadhaa nje ya nchi na pia nina kazi yangu serikalini nimeajiliwa lakini nilisimama imara na kumuomba mungu na kweli leo nakula kivulini. Unajua zamani zanzibar mimi sikuwa lolote mbele ya Latipha salum muimbaji mwenzangu lakini hilo halikunikatisha tamaa niliendelea kupambana na kuonyesha umahiri wangu kwenye kuimba sikukata tamaa na mwisho wa siku leo hii namshukuru mungu nimefika hapa nilipo, sasa khadija mbegu namuasa kwanza awe mvumilivu na aongeze juhudi asiridhike na kiwango alichonacho cha uimbaji wake ajifunze zaidi na zaidi, mimi namkaribisha unguja akipata nafasi anaweza kuja maana kule ni kama chuo kwa uimbaji wake akikaa miezi michache na kurudi huku bara watu watamshangaa zaidi, nampongeza sana huyu msichana ana kipaji kikubwa sana mimi najua alimaliza kwa kusema Saada nassor.

Saada nassor alialikwa kuja kuimba hapa dar es salaam katika bendi bora ya gusagusa ndipo alipoweza kukutana na msichana huyu mdogo, mwembamba, akiwa ktk jukwaa la bendi hiyo, juhudi za kumtafuta khadija mbegu mwenyewe ili azungumzie pongezi hizi alizopewa na muimbaji nguli Saada nassor anazizungumziaje zinaendelea na tutawaletea humu humu mtandaoni.

Ijumaa, 17 Novemba 2017

22:45

HAMISI MAJALIWA:- SINA MUDA WA KUJIBISHANA NA YEYOTE MITANDAONI.

Na pambe za taarab.

Mkurugenzi wa maja's modern taarab Hamisi majaliwa amezungumza na mtandao huu wa pambe za taarab na kusema kuwa hana muda mchafu wa kujibishana na yeyote katika mitandao, mimi naangalia bendi yangu wapi inaelekea nini nifanye ili niweze kuboresha maisha ya wasanii wangu.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo pale alipoulizwa swali kuwa anazungumziaje tuhuma alizoshutumiwa na aliekuwa msanii wake Amina mnyalu ambae kwa sasa yupo kwenye bendi ya Yah tmk modern taarab, mnyalu alisema aliwahi kupigwa sana na majaliwa wakati wanatoka safari na maja's modern taarab na sababu ilikuwa ni baada ya mgeni kisoda Kuchukuwa pesa za majaliwa lakini kwenye kusafiri akaingia mitini na mnyalu ndie ambae alikuwa mdhamini wa kisoda kwenye kupewa pesa hizo.

Majaliwa alianza kwa kusema, mimi sio mtu wa kujibishana ktk mitandao na hata kama huyo Amina anasema kuwa mimi niliwahi kumpiga nadhani mngeenda kuuliza polisi maana hiyo ni kesi, mimi sina la kusema sipo tayari kumpa mtu kiki, na anaposema kuwa hayupo tayari kurudi maja's kwani nani kasema anamtaka?, mimi katika bendi yangu wala simfikirii kabisaa! katika majina ya wasanii. Unajua kuna majina ya wasanii ambao naamini hawa walikuwa muhimu kwangu na kwa bendi yangu ya maja's modern taarab mfano Young hassan ally, kibibi yahya, khanifa maulid, Marehemu nyawana fundikila, Aisha vuvuzella, mrisho rajabu, mwajuma kidoti, salha abdallah na senior bachelor hawa ndio wasanii ambao walipitia maja's na wengine bado wapo mpaka sasa na walikuwa na wana umuhimu mpaka leo kwangu na kwa bendi yangu hii, lakini mtu kama huyo Amina mnyalu wala sina muda na yeye sababu najua uwezo wake mdogo sana kwenye kuimba alisema majaliwa.

Habari hii ni kama mrejesho wa ile habari ambayo tuliwahi kuiandika hapa juu ya Amina mnyalu kusema yeye hana muda wa kurudi tena maja's modern taarab hata aambiwe bure ni bora kama bendi zote zimekwisha atauza biashara zake ndogondogo tu na hii ni baada ya kupigwa na mkurugenzi wake huyo.

Ijumaa, 10 Novemba 2017

20:14

NYAWANA FUNDIKILA, NI MIAKA MINNE SASA UMETANGULIA MBELE YA HAKI.

Na kais mussa kais.

Waswahili wanasema msiba uusikie kwa mwenzio!, pale inapofikia kipindi mwenza wako ambae mlikuwa mkishauliana, mkila pamoja, mkijifunika shuka moja, mkikoga pamoja, mkicheza na kutaniana matani ya hapa na pale anapoiaga dunia tena kwa kifo cha ghafla kwa kuumwa siku mbili tu! machungu yake yanakuwa hayasemeki kiukweli.

Nyawana umezimika kama mshumaa pembezoni mwa upepo wa bahari huku ukiwa bado unahitajika sana na jamii inayokuzunguka nikiwemo mimi mumeo!, ni mengi tuliyazungumza na kuyapanga yakiwemo ya kimaisha na mengineyo lakini hayakutimia mwenyezimungu aliamua kukuchukua na kutangulia mbele ya haki, sina nitakalo lisema zaidi ya kukuombea dua na kumuomba Allah akupe kivuli miongoni mwa vivuli vya peponi inshallah.

Tarehe kama ya leo mida ya saa saba mchana ukiwa kitandani kwetu uliniaga dunia na kuniachia usia ambao sitokaa nikusahau, nakumbuka uliniambia "kais mume wangu, mimi nakufa lakini nakufa nikiwa nakupenda sana! roho yangu inauma kwakuwa najua utapata shida sana kwakuwa mapenzi yetu ni ya dhati na hakuna ambae anapenda kuwa mbali na mwenzie" kauli hii inaendelea kujirudia masikioni mwangu kila wakati...mungu akurehemu na akusamehe madhambi yako kwani naamini ipo siku tutaja onana tena.

Kikubwa napenda ujue kwamba Nakukumbuka sana, nakufanyia sana visomo vya dua ili Allah akufanyie wepesi katika mitihani yako, siku zote kazi ya mungu haina makosa, lala salama Nyawana, mashabiki, wapenzi, wadau viongozi mbalimbali wa taarab, watoto wako, ndugu jamaa na marafiki pamoja nami mumeo tumekuwa mstari wa mbele kukukumbuka na kufanya dua kwa ajili yako, hii yote ni kuonyesha mapenzi ya dhati tuliyonayo kwako...mwisho kabisa nasema upumzike kwa amani nyawana isale fundikila kwani siku na wakati wowote nasi pia tutakufa kwani kila kilichozaliwa na kupewa pumzi basi siku ikifika kitakufa. Mwenyezimungu akurehemu inshallah.

Jumatano, 8 Novemba 2017

12:14

AMINA MNYALU:- KAMWE SIWEZI KURUDI MAJAZ MODERN TAARAB...HATA BURE!!.

Na pambe za taarab.

Muimbaji chipukizi anaefanya vizuri kwa sasa ndani ya bendi ya Tmk modern taarab Amina rashid a.k.a. Amina mnyalu ametoa la rohoni kwa kusema kuwa kamwe hayupo tayari kufanya kazi tena ndani ya bendi yake ya zamani ya majaz modern taarab.

Akizungumza na wadau ktk group la whatsap liitwalo pambe za taarab kwenye kipengele kiitwacho sindano za motto ambacho huwa kinakuwa hewani kila siku za jumatatu Amina aliongea hayo baada ya kuulizwa swali kuwa wakati majaz wapo safarini mpanda ilitokea sintofahamu akapigwa makofi na mkurugenzi wake je ni kweli?, ndipo Amina akaeleza  habari hizo ni kweli na kisa cha mimi kupigwa ni stori ndefu sana lakini sitoweza kuizungumzia, ila kwa tukio lile nimeapa kwamba kamwe haitotokea mimi kurudi tena kufanya kazi ktk bendi ile hata kama bendi za kwenda ziwe zimekwisha basi nibora nifanye biashara zangu tu.

Mwandishi wa habari hizi alijaribu kumtafuta mkurugenzi wa majaz ktk simu yake lakini hakupatikana hewani tutajitahidi kumtafuta ili tuweze kuwaletea nae anasemaje juu ya haya aliyoyazungumza Amina mnyalu yana ukweli kwa kiasi gani...tuendelee kuwa pamoja wasomaji wetu.