Muimbaji wa taarab toka katika bendi ya Supershine Modern Taarab Issa Kamongo, siku ya tarehe 25/10/2014 jumamosi alifunga ndoa na binti aitwae Hafsa maeneo ya ilala na kufuatia sherehe kubwa iliyofanyika nyumbani kwao kariakoo jijini Dar

Aliposhuka yeye akapanda Mussa Kijoti ambae nae aliimba wimbo mmoja, wasanii wengine kama Ndagendage, Omary Kisila, Mussa Mipango, Ally J walishiliki pia kupiga vyombo wakati bendi ya Supershine ikifanya yao.
Harusi hiyo ilipata baraka ya kuhudhuliwa na watu wengi maarufu na wakurugenzi wa mabendi kama Dokta No! wa supershine, Hamisi Slim wa G5, Senior Bachelor wa Bongo Stars Modern Taarab, pia watangazaji wanaotamba mjini kwa sasa kama Mwanne Othman wa East Africa Redio, wadau maarufu kama Mc Nora Kyando, Rajabu Magomba, Mama Zeka, Mama Double S, Mc Mchafuko, Mc Bonge, Rukia Kuffi, Halima Temu na wengine wengi..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni