Wimbo uliokuwa unasubiliwa kwa hamu kubwa toka kwa Mariam B.s.s. akiwa na bendi nzima ya 5 stars modern taarab uitwao "Kichambo kinakuhusu", umeachiwa rasmi jana jumapili katika vituo mbalimbali vya redio nchini, na hii ni katika kuwathibitishia wadau na wapenzi ujio mpya kabisa wa bendi hii ya 5 stars inayoongozwa na Ally J.

Pia kwa siku ya jana 5 stars wameachia na wimbo mpya kabisa wa Mussa Kijoti uitwao Big up my dear!. ambao ni matata mno!. Huu ni ujio mpya kabisa wa bendi hii wadau na wapenzi mnaombwa kuwasapa sapoti ili waweze kufanya mambo mazuri zaidi ya haya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni