
Akizungumza na mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com, Kais alisema show ya leo si ya kukosa kwani kuna mambo mengi mazuri yameandaliwa kwa ajili ya mashabiki ikiwemo zawadi kwa atakae pendeza zaidi ya wote.
Aliwaomba wadau na mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kupata burudani ya nguvu toka kwa watoto wa magomeni. Supershine kwa sasa inatesa na album ya HUNA STYLE iliyo na nyimbo tano ambazo ni Usia wa baba, iliyoimbwa na Queen Salma akishilikiana na Ally Mikidadi, Wafadhilaka, iliyoimbwa na Nuru Moshi, Nimempata wa ukweli, iliyoimbwa na Ally Mikidadi, Hunishtui, iliyoimbwa na Zainabu Mteza pamoja na Huna style yenyewe ambayo imeimbwa nae Queen Salma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni