TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 16 Agosti 2015

DOGO JACK SIMELA:- MUZIKI WA MCHIRIKU UNAHITAJI SAPOTI KUBWA TOKA KWA VYOMBO VYA HABARI.



Pengine ni muziki unaotambulisha taifa la Tanzania nchi nyingine hususani bara la Ulaya kuliko muziki wowote kutoka hapa nchini. Lakini cha ajabu aina hii ya muziki “Mchiriku” hapa nyumbani sio muziki unaovuma na kujulikana kama muziki wa bongo flava.

Kwa mujibu wa mwanamuziki ambaye anauwezo wa kupiga vyombo kadhaa vya muziki na muimbaji hodari wa mchiriku Jack Simela a/k/a Dogo Jack kutoka kundi la muziki huo Jagwa amesema miaka ya 1990 na mwanzoni mwa 2000 Mchriku ulikuwa juu sana hapa nchini sio tu kwa sehemu za uswahilini bali hata sehemu za ushuwani watu waliuelewa muziki huo.

DOGO JACK SIMELA.

Bendi za Mchiriku ambao kwa jina jingine unatambulika kama mnanda zilizokuwepo kipindi hicho, Atomic, 7 Survivor, Jagwa, Cha Ukucha na Dege la Jeshi zilikuwa na ushindani mkubwa sana.

Dogo Jack amesema mambo yamebadilika siku hizo na watu wanafuatila zaidi muziki wa bongo flava kuliko muziki wao kitendo ambacho kinafanya wasanii wengi wa mchiriku kugeukia soko la muziki wa Bongo flava na kuachana Mchiriku.

Dogo Jack amefunguka wazi kuhusu show zao wanazopiga nje ya nchi mfano bara la Ulaya kwamba haziwalipi.

DOGO JACK SIMELA AKIFANYA YAKE STEJINI.

“Ni kweli tunafanya show nyingi nje ya nchi lakini hazitulipi, wanaotusimamia wanatulipa fedha kidogo sana ambazo hata kujikimu kwa mahitaji yetu ya kifamilia hazitoshelezi”, alisema Dogo Jack.

Pia muimbaji huo alitoa ushauri kwa wadau wa tasnia ya muziki nchini kujaribu kuwasaidia wanamuziki wa mchiriku kuufanyia promo muziki huo ili uweze kurudi upya kwani asilimia kubwa ya nyimbo zao zina ujumbe mkubwa kwa jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni