TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 20 Agosti 2015

HASHIM SAIDI "IGWEE" AJIENGUA MASHAUZI CLASSIC NA KUJIUNGA NA WAKALIWAO MODERN TARADANCE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Wadau wanasema kuwa wakaliwao modern taradance kwa sasa imekuwa tamu kama mcharo!, kauli hii inakuja baada ya aliekuwa Director wa mashauzi classic Hashim said "igwee" kujiunga na bendi hiyo akitokea mashauzi classic modern taradance.

KAIS MUSSA KAIS NA HASHIM SAIDI.

        Ilikuwa kama movie tamu yenye muendelezo kulingana na wakaliwao modern taradance walivyofanikiwa kumnyakua muimbaji huyo mwenye kipaji hapa nchini, alipokuwa anatoka redio times kufanya mahojiano na Dida, viongozi wa bendi ya wakaliwao yaani kais mussa kais, thabit abdul na ally tiketi walimnyakuwa juu kwa juu na kumuweka katika gari la kifahari lenye vioo vya tintedi na kwenda nae hotelini tayari kwa mazungumzo, mazungumzo yao yalichukuwa takribani masaa matatu mpaka muafaka kupatikana na picha kadhaa wa kadhaa kupigwa na kurushwa katika mtandao.


THABIT ABDUL NA HASHIM SAIDI.

    Hashim saidi akizungumza kwa furaha baada ya kukamilika kwa zoezi hilo alisema nimefurahi sana kujiunga na wakaliwao modern taradance kwani ni bendi niliyokuwa naipenda tokea kitambo kulingana na utendaji wa thabit abdul, ikumbukwe kuwa nilishawahi kufanya kazi na thabit abdul pale mashauzi kwahiyo najua utendaji wake.

ALLY JUMA NA HASHIM SAIDI.

       Hashim saidi anatarajiwa kupanda jukwaa la wakaliwao modern taradance kwa mara ya kwanza kesho ijumaa katika show ya wakaliwao itakayofanyika pale JM HOTEL manzese jijini dar, wadau, mashabiki na wote wanaoipenda wakaliwao wanaombwa kufika kwa wingi kumuona Hashim saidi akiwajibika steji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni