INTRO / CHORUS.
Twaliombea salama, Taifa letu tanzania
Amani yetu idumu, Daima milele
Tudumishe muungano, Upendo na mshikamano
Tuingie awamu ya tano, Bila ya mifarakano
Mwananchi jitokeze, Ukapige kura yako
Fursa usiipoteze, Kupiga kura haki yako
VERSE:- 1
Ombi letu msikie, enyi wote viongozi wa vyama vyote nchini
Msifanye kampeni, kwa lugha za uchokozi, zitahatarisha amani
Maendeleo tunayoyataka, nguzo yake ni amani
Tuilinde isije toweka, tukawa mashakani.
VERSE:- 2
Shime wazee kwa vijana, tukapige kura kwa amani
Kisha turudi majumbani, tusiweke vigenge mitaani
Tuipokee awamu ya tano, bila ya mifarakano
Utamaduni wa mtanzania, ni upendo na mshikamano.
VERSE:- 3
Mwananchi utambue, thamani ya kura yako
Umtakae mchague, mwenyewe kwa siri yako
Tusichague kwa udini, ukanda wala ukabila
Tanzania yetu ni moja, na watu wake ni wamoja.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA!.
MTUNZI:- EL-KHATIB JOB.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni