TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 30 Oktoba 2015

15:10

USAILI WA WASANII WAPYA WA WAZAWA MODERN TAARAB NI TAREHE 2/11/2015 PALE CCM MWINYIJUMA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


               Usaili wa wasanii wapya wa bendi ya wazawa modern taarab utafanyika siku ya jumatatu saa nne asubuhi katika ukumbi wa ccm mwinyijuma uliopo mwananyamala A jijini dar.

THABIT ABDUL MRATIBU WA USAILI HUO WA VIJANA!.


           Akizungumza na mtandao huu makini mratibu mkuu wa usaili huo thabit abdul amesema kuwa anahitaji vijana wenye vipaji na ambao watakuwa tayari kufanya kazi katika mazingira yoyote yale, huu ni mwanzo tu lakini nia kubwa haswa ni kusaidia vijana na mambo yakiwa mazuri zaidi malengo yangu ni kufungua chuo kabisa kwa ajili ya kufundisha muziki huu wa taarab hapa nchini.


          Katika usaili huo vijana watakao patikana wakike na kiume watajiunga moja kwa moja na bendi hii na kuingia kambini tayari kwa kufundishwa na kufanya show ambazo zipo na bendi hii tayari. Napenda nichukue nafasi hii kuwatoa wasiwasi wadau na wapenzi wa wakaliwao modern taradance kuwa wasiwe na hofu, bendi hii haitoingiliana na shughuli za wakaliwao...mimi mwenyewe mpaka naianzisha bendi hii nimeangalia hayo na nimeyapatia ufumbuzi.kwahiyo nawakaribisha vijana wote wenye vipaji kufika katika usaili huo saa nne asubuhi pale ccm mwinyijuma siku ya jumatatu tarehe 2/11/2015 bila kukosa hii ni nafasi adhimu hivyo itumieni kwa ufasaha alimaliza kwa kusema.

11:42

MZEE YUSUPH ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS MTEULE JOHN POMBE MAGUFULI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                  Mkurugenzi wa Jahazi modern taarab mzee yusuph ametuma salamu za pongezi kwa muheshimiwa magufuli kwa kufanikiwa kushinda kiti cha urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini tarehe 25/10/2015.

MZEE YUSUPH.

              Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mzee yusuph alisema nimefurahishwa sana zaidi ya sana kwa ushindi wa muheshimiwa magufuli na chama cha mapinduzi kwa ujumla, nikiwa kama mwanachama wa chama cha mapinduzi nampongeza sana rais wetu na kilichobaki kwake ni kazi tu kama ilivyo sera mama ya chama chetu "hapa kazi tu". Pia naamini muheshimiwa ni mpenda sanaa na michezo sana tu, kwahiyo nina imani kwa asilimia kubwa wasanii na wanamichezo watanufaika sana kwa kipindi chote cha utawala wake alimaliza kwa kusema!.

Alhamisi, 29 Oktoba 2015

14:13

HIVI ULIKUWA UNAJUA KUWA "NASEMA NAWE" YA DIAMOND PLATINUM IMETENGENEZWA NA ALLY J?.

NA KAIS MUSSA KAIS.

         Hivi ulikuwa unajua kuwa wimbo "nasema nawe" ulioimbwa na Diamond platinum na kupata sifa kubwa miongoni mwa mashabiki hapa tanzania na afrika nzima kwa ujumla umetengenezwa nae Ally J, mkurugenzi wa five star's modern taarab?.

ALLY J-MKURUGENZI WA FIVE STAR'S MODERN TAARAB.

       Basi kama ulikuwa hujui habari ndio hiyo!, akizungumza na mtandao huu makini wa taarab afrika mashariki kwa sasa! Ally J alisema kuwa ni kweli ndugu mwandishi wimbo ule nimeutengeneza mimi kwa kupiga kinanda na pia nimepiga gitaa la besi ila uimbaji "melodies" amekuja nazo mwenyewe Diamond isipokuwa kuna baadhi ya mistari tulikuwa tukirekebisha kwa pamoja. na tumeirekodi kwa producer aitwae "Tuddy thomas".

ALLY J AKIWA NA ISSA KAMONGO WAKIHOJIWA.

        Mwandishi alitaka kujua thamani ya pesa aliyolipwa na diamond baada ya kurekodi wimbo nasema nawe, alilipwa kiasi gani? maana kuna taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa Ally J alilipwa milioni mbili je ni kweli?, akijibu swali hili Ally J alisema, kiasi nilicholipwa na diamond baada ya kurekodi wimbo huu bado itakuwa ni siri yangu ila kwa ufafanuzi kiasi ni kwamba alinipa pesa nyingi ambayo hata kama ningechukuliwa na mtu yeyote ili nirekodi albam nzima ya taarab asingeweza kunilipa pesa kama ile! kifupi namshukuru sana diamond na namkaribisha tena siku ingine ili tufanye kazi nzuri zaidi alimaliza kwa kusema!.

12:49

QUEEN SALMA, NYOTA YA SUPERSHINE MODERN TAARAB ISIYOCHUJA DAIMA MILELE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


              Unapoizungumzia bendi kongwe ya taarab nchini tanzania, supershine modern taarab, basi ni lazima ulitaje jina la Queen salma nyota isiyochuja ndani ya bendi hiyo.


QUEEN SALMA AKIIMBA SAMBAMBA NA ALLY MIKIDADI.

          Huyu ni mke halali kabisa wa mkurugenzi wa bendi hii anaejulikana kwa jina la Dr no! au "mzee wa ukwaju". Ukipata bahati ya kuhudhuria onyesho lolote la bendi hii basi utafurahi na nafsi yako pale anapotangazwa na mc wa bendi Issa kamongo kwamba anaekuja kuimba sasa ni Queen salma, sauti tamu, haiba, tabasamu na manjonjo anapokuwa anaimba ni moja ya sababu inayomfanya aendelee kuwa juu na kupendwa sana na mashabiki wake!.


QUEEN SALMA.

        Queen salma ni mwalimu wa muziki huu wa taarab na asilimia kubwa ya waimbaji wa taarab wamepitia mkononi mwake kwa kuwafundisha na sasa wamekuwa maarufu sana!, Queen salma ameanzia mbali sana sanaa hii tokea akiwa egypsheni club bendi iliyokuwa na wakongwe kipindi hicho cha nyuma! amekuwa pale kwa muda mrefu mpaka mumewe Dr no! alipoanzisha bendi hii ya supershine modern taarab na kumkabidhi mkewe kwakuwa aligundua kipaji anacho na anafaa kuendelezwa zaidi.


QUEEN SALMA.

      Ukitaka kuishuhudia bendi hii ikifanya mambo yake na kumuona Queen salma akiiongoza vyema supershine modern taarab, basi tembelea magomeni mwembe chai flamingo night club kila jumatano wanapiga pale na pia kila jumapili wanapiga Royal mwananyamala kwa mama zakalia, nenda ukamuone Queen salma nyota isiyochuja daima!.

11:23

HAMUYAWEZI KONDO:- SINA MPANGO WA KUIHAMA WAKALIWAO MODERN TARADANCE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


           Hamuyawezi kondo "mamaa wa kalieni viti sio umbea" muimbaji wa wakaliwao modern taradance amevunja ukimya kulingana na maneno yanayo endelea kuzungumzwa na wadau kwamba yupo katika mazungumzo na uongozi wa bendi ya moyo modern taarab ili ajiunge nayo!.


HAMUYAWEZI KONDO-MUIMBAJI WAKALIWAO.

        Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake na kumjulia hali mtoto wake, Hamuyawezi alisema mimi sina mpango wa kuihama wakaliwao modern taradance kabisa huu ukimya wangu ni sababu nipo katika likizo ya uzazi tu kwani nimejifungua hivi karibuni, nimekuwa nikisikia toka kwa wadau eti mimi nataka kwenda kujiunga na bendi ya moyo modern taarab, hii habari sikweli, kwanza hata hao viongozi wa bendi hiyo siwajui na hawajawahi kunipigia simu...!, sijui kwanini nimekuwa nikizushiwa habari hii alihoji?.


      Hamuyawezi kondo ni muimbaji mwandamizi wa wakaliwao modern taradance na mpaka sasa ameshaimba nyimbo mbili katika bendi hiyo ambazo ni, kalieni viti sio umbea na ingine inaitwa mtu mzima ovyo, ambazo zimekuwa zikiendelea kufanya vizuri katika media mbalimbali afrika mashariki na kati.

Jumatatu, 26 Oktoba 2015

15:37

MWINYI MKUU NA MAINA THADEI, WAAHIDI KUFANYA MAKUBWA NDANI YA MACHOKODO BAGAMOYO TAREHE 30/10/2015.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                Mwinyi mkuu na maina thadei ni wasanii wanaofanya vizuri sana kwa sasa katika tasnia hii ya taarab hapa nchini, wimbo uliowatambulisha katika tasnia hii ni "shida simu".

           Siku ya ijumaa tarehe 30/10/2015 watakuwa na show bab-kubwa itakayofanyika bagamoyo mkoani pwani katika ukumbi wa machokodo, show hii ambayo imedhaminiwa na cloud's Tv chini ya kipindi cha ng'aring'ari kinachoongozwa na sakina lyoka itakuwa ni ya kukata na shoka, watoto wa mjini wanakwambia "hatumwi mtoto dukani". kwakweli nimepania kufanya show ya nguvu kwani wakazi wa bagamoyo wamekuwa wakinipa sapoti kubwa sana katika kazi zangu alisema maina thadei.

        Nae mwinyi mkuu kwa upande wake alijinasibu kwamba amekuwa akifanya mazoezi ya nguvu rasmi kwa ajili ya show hiyo, so! amesema yeye hana maneno zaidi ila kilichopo anawaomba wadau na wapenzi waje kwa wingi siku hiyo wajionee excellent modern taarab nini tumewaandalia.kiingilio siku hiyo ni shilingi elfu 6000 tu kwa mtu mmoja na milango itakuwa wazi kuanzia saa mbili usiku.

02:51

MMEIUA TAARAB ASILIA, MNASAPOTI TARADANCE NA KUIITA TAARAB MNASHANGAZA SANA!.

Na pambe za taarab
Pambezataarab@gmail.com
     

                    

                          Muziki wa taarabu una asili na fasili yake katika watu wa pwani na visiwani na maeneo ya mwambao wa Afrika Mashariki.

Umeathirika kwa kiasi kikubwa na muziki wa Mashariki ya Kati, India na kaswida za Kiislamu.


Sifa moja kubwa ya muziki wa taarabu tofauti na wengi wanavyofikiri sio maneno na mpangilio wake, bali ala za muziki huo na mipangilio yake na ule ufundi wa kila mwanataarabu kuwa bingwa au stadi katika kupiga chombo fulani. Taarabu isipokuwa na ala hizi sio taarabu ni igizo tu kwa kiasi fulani la kitu kama taarabu. Taarab kwa kawaida ni kitulizo cha fikra ndani ya nyumba na katika hadhara isiyoshawishiwa na usasa na umagharibi kiasi cha kupuuza maadili na mila za wahusika.


Ala za taarabu ni nyingi na swahiba wangu El-hatibu rajabu ambaye sio tu shabiki wa taarabu bali ni mtunzi pia wa nyimbo za taarab anaweza baadaye kunipokea hapa na kuelezea zaidi kwanini tunastahili kuwekeza kwenye taarab asilia kama eneo la utamaduni linalostahili kuhifadhiwa na kuenziwa.


Taarabu kama walivyoiendelza kina Siti binti Sadi, Bi Kidude, Juma Bhalo na kina Sheikh Ilyas, Machapurala bila kuwasahau mamia ya wanawake na wanaume wa Kizanzibar na Kimrima waliochangia maendeleo ya tasnia hii adimu lakini iliyo na sifa ya kuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa mwambao ya Pwani ya Afrika Mashariki na usiostahili kuachiwa kupotea.


Taarabu ni muziki wa enzi na enzi. Ni sehemu ya utamaduni endelevu na hususan katika mikoa ya pwani ya Afrika Mashariki. Taarab ni ustaarabu, utaratibu, upole na uungwana. Taarabu ni kitulizo cha mawazo na gundi ya kuunganisha familia kama sio ukoo mzima. Sifa ambayo si mipasho, sio rusha roho sio mnanda unayo.


Taarab kiasili sio muziki wa kucheza bali wa kutazama, kusikiliza, kutafakari na kutunza. Huu ni muziki uliokuwa ukisikilizwa na watu wenye fikira, busara na hekima kuwapa muda wa kuwaza na kuwazua juu ya hili au lile. Muziki wa kupayuka, kujiona, mashauzi, kusemana, kutukanana, kuumbuana na wenye nyimbo ambazo hazina staha, usiri wala taadibu ya kuimbwa katika mafumbo hauwezi kuitwa taarab.


Ni muziki ambao kwa kawaida una ala takriban ya ishirini. Na kwa wapenzi halisi wa taarabu hufuatilia upigaji wa kila ala na ufundi au ugwiji wa yule anayetumia ala husika. Aidha, mashairi ya taarab hayaangalii tu mlingano wa vina na mizani bali maudhui na mantiki ya kile kilichomo tena kikiwa kwenye mafumbo kuweza kusomeka vyema na wanaosikiliza wimbo husika.


Ni muziki ambao hutungwa kwa mafumbo na kwa namna ambayo hauzuii familia nzima, yaani, babu, bibi,baba,mama, kaka na dada wote kujumuika kwa pamoja bila kutokea chochote ambacho kinaweza kuwafanya washindwe kuzungumza au kutazamana. Taarab kiasili uliunga pamoja familia za wakazi wa mji husika. Tofauti na hiyo inayoitwa 'modern taarab' au 'taradance' ambayo kwa kiasi kikubwa inazivunja familia katika kila mji na kijiji.


Siti bint Saad (1928) ndiye nyota wa kwanza wa taarab

ambaye kwa mara ya kwanza badala ya kuimba kwa Kiarabu aliimba kwa Kiswahili. Alifyatua mamia ya santuri za nyimbo India na wapenda muziki wa enzi hizo hakuna aliyekosa wimbo wake nyumbani.


Muziki wa taarab asili hauna tofauti na 'Classical Music' wa Ulaya au 'Country Music' wa Marekani. Miziki hiyo ilikuwepo, imekuwepo na itakuwepo bila kubadilika wala kuitwa kwa jina jingine wala kupigwa kwa namna nyingine tofauti na ilivyokuwa, ilivyo sasa na itakavyokuwa kesho.

Ni sehemu ya kudumu ya utamduni wa watu na sio kitu cha kupita na kusahaulika.


Aina hizo za miziki pamoja na kuzuka kwa miziki ya kila aina Ulaya na Marekani bado inatambulika kwa nembo na jina lake. Country ni country na classical ni classical. Hapajakuwepo muziki mwingine uliopewa umodern kuhusiana na miziki hii, hakuna kitu kama modern country au modern classic.


Rouget katika Music and Trance anafafanua kwamba neno taarab linatokana na neno la kiarabu 'tariba' likiwa na maana ya hisia za kusisimka, kudhihirisha au kutaka kufanya kitu fulani kama vile kuimba au kucheza taarab.


Taarab asili ilingia kwanza hapa Afrika Mashariki kupitia Zanzibar kunako miaka ya 1870. Aliileta Sultan Seyyid Barghash ambaye alileta kikundi cha wanamzuki toka Misri kukaa kwenye jumba lake la Kifalme.


Tofauti na viongozi wetu wa leo, Barghash aliwapeleka Wazanzibari kadhaa wakiongozwa na IbrahimMohammed kwenda kusomea muzki nchini Misri nao waliporudi waliunda kikundi cha kwanza pengine cha taarabu Afrika Mashariki kilichoitwa Zanzibar Taarab Orchestra.


Kunako 1905 kikundi cha pili cha taarabu kilizaliwa huko huko Unguja kikiitwa Ikwhani Safaa Musical Club. Kikundi hicho kipo hadi wa leo, lakini kama vilivyo vikundi vingine vya taarab 'hasa' havina msaada wowote wa maana toka kwa yeyote yule, kwani inavyoelekea wengi pamoja na viongozi wa serikali wametekwa na rusharoho na mipasho.


Taarab asili haistahili kuonekana kama ni taarab tu. Ni zaidi ya taarab. Hii ni hazina ya utamaduni katika mwambao wa Afrika Mashariki kuanzisa Lamu hadi Kilwa na Sofala.

Kama jitihada zinavyofanyika kukarabati na kutunza maeneo kama vile Mji Mkongwe Zanzibar, Bagamoyo na Kilwa ili iendelee kuwepo basi upo umuhimu pia wa wanaohusika katika serikali zetu kuhakikisha kuwa muziki wa taarab asili na wanamuziki wake wanakumbukwa na kuenziwa na kisha kizazi kipya kinajengwa ili kuendeleza muziki huu kwa faida ya vizazi vijavyo. Kwa maana, ukweli ni kwamba taarab asili ikipotea ndio utakuwa mwisho wa taarab hapa Afrika Mashariki.


Kwanini tuhifadhi taarab asilia?


Kwa bahati mbaya wengi tumezoea kuchukulia vitu kama ardhi, fedha, nyumba, magari kuwa ndio rasilimali tu. Lakini muziki wa kiasili nao ni rasilimali muhimu kimaendeleo na kisaikolojia. Bila urithi wa namna hii tutakuwa ni taifa lipolipo tu ambalo si jambo zuri.


Pamoja na mambo mengine kuifufua, kuitunza na kuiendeleza taarab asili ni jambo lenye faida kadhaa ikiwemo kuendeleza mila na utamaduni wetu; kuzileta familia pamoja mara kwa mara; kujenga maadili bora katika jamii; kuwa na muziki usioendana kinyume na maadili ya dini; kukuza na kuendeleza ushairi na Kiswahili; kuwa kivutio kwa wageni wa leo na kesho

na kuzienzi na kuendeleza ala asili za muziki na upigaji wake.

 

Miziki inayojiita modern taarab iitwe kwa majina yao yanayostahili kama ni kiduku basi kiduku, kama ni rusha roho basi rusha roho fulani, kama ni mipasho basi ni mipasho na kama ni mnanda uitwe mnanda
na miziki hii isiruhusiwe kutumia mgongo wa taarab kujijenga isipostahili.

Nikiri kuwa nilitaka sana nitembelee Lamu, Malindi, Mombasa, Tanga na Zanzibar kuzungumza na wakereketwa wenzangu wa taarabu asili kabla ya kuandika makala haya lakini haikuwezekana. Ninaamini, hata hivyo kupitia makala haya ujumbe unaweza kufika kwa kiasi fulani.

Ninawashauri wanaharakati wa kulinda na kuendeleza utamaduni wetu kuangalia uwezekano wa haya yafuatayo: Kusaidia juhudi binafsi zilizopo za kufufua na kuendeleza vikundi vya taarabu kupitia vilabu na vyuo vya upigaji ala za asili za taarab (mathalani juhudi za Bi Hamdani, Zanzibar) ; Kushirikiana na UNESCO kuhifadhi taarab asili kwa kutumia TEKNOHAMA;
Kuwatafuta wanataarab asil waliko na kuwaunganisha ili kuufufua na kuchochea kuwepo kwa muziki huo kiasili na kuongeza vionjo viwili vitatu vya kuvutia familia zaidi kuliko mtu mmoja mmoja.

Aidha, kusaidia vikundi vilivyopo lakini havina ala za kutosha za muziki toka Misri na Uarabuni; kuenzi Ushairi katika vyombo vya habari kukuza vipaji vya washairi chipukizi na
kuchukulia Taarab asili kama urithi usiostahili kupotea kwa msaada wa UNESCO na wapenda utamaduni wetu wengineo.

Baada ya Watanzania kugeuka wavivu wa kila kitu ikiwemo kupiga ala za muziki na kutaka mteremko katika kila jambo wale waliozuka na mitindo inayotumia mashairi au tungo zenye vina na mizani au isivyo hivyo wakaona urahisi ni kuita miziki yao 'modern taarab' au 'taradance'. Miziki hiyo ninakaata sio taarabu bali inastahili kuitwa mipasho, kiduku, rusha na roho au mnanda na vitu kama hivyo lakini sio kamwe taarab.

Jumapili, 25 Oktoba 2015

09:06

HASHIM SAID:- MIMI SIO "MALIOO", KAZI YANGU NI MUZIKI, NAENDESHA FAMILIA YANGU KWA MUZIKI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


         Hashim said igwee ni mwanamuziki wa bendi ya wakaliwao modern taradance na amekuwa akifanya vizuri sana katika tasnia ya taarab nchini.


HASHIM SAID IGWEE!

       Kumekuwa na maneno maneno yakiendelea kuzungumzwa na walimwengu kwamba hashim said ni mtu ambae amekuwa akipenda sana kulelewa "malioo" na wanawake zake ambao anakuwa nao kimapenzi, katika kuliweka sawa jambo hili, hashim saidi amekanusha habari hii wakati akifanya mahojiano redio cloud's fm kwenye kipindi cha leo tena akiwa na watangazaji mussa hussein, geah habibu na husna b.


       Nashangazwa sana na maneno haya ambayo yamezagaa karibu dar nzima juu ya mimi kuitwa "malioo", mimi ni mwanamuziki na napata ridhiki zangu kwa kazi hii kwanini mtu anaamua kunichafua kwa kunipa udhaifu huo? alihoji hashim said. nawaomba waniachee na familia yangu na pia kuanzia sasa waache kabisa kunizushia upuuzi huo.

HASHIM SAID IGWEE!.


          Ninayo sauti ambayo niliirekodi wakati hashim said akihojiwa na kukanusha kuwa yeye sio "malioo" au mwanaume ambae analelewa na wanawake, nitaiweka hapa mtaisikiliza akihojiwa sambamba kabisa na mkewe zainab manyeko.

07:34

YOUNG HASSAN ALLY:- NI KWELI MOYO MODERN TAARAB WALINIFUATA LAKINI............!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


              Wiki moja iliyopita mtandao huu ulilipoti habari kuwa young hassan ally yupo mbioni kujiunga na bendi ya moyo modern taarab inayoongozwa na mkubwa fellah akitokea ogopa kopa, lakini leo hassan ally ametolea ufafanuzi habari hiyo kama ifuatavyo.


YOUNG HASSAN ALLY!.

          Ni kweli ndugu mwandishi, hawa jamaa wa moyo modern taarab wamenifuata wakitaka nijiunge nao na sio wao tu ipo bendi ingine kubwa na yenye jina pia nimefanya nao mazungumzo, lakini ukweli ni kwamba mpaka sasa mimi ni msanii wa ogopa kopa classic bendi, nikiwa na maana kwamba hatujafikia muafaka wa mimi kujiunga nao kwani mahitaji yangu niliyowabainishia kuyahitaji toka kwao bado hawajanikamilishia. mimi ni msanii  na sanaa ndio kazi niliyoichagua kuniendeshea maisha yangu, pamoja na ubinadamu lakini mwisho wa yote maslahi ndio kitu muhimu nafikili nitakuwa nimeeleweka ndugu mwandishi.


            Ikumbukwe kuwa young hassan ally pamoja na kuwa muimbaji mzuri lakini pia ni mtunzi wa mashairi na vile vile ni director ambae anaweka sauti na kubuni muziki wa wimbo husika anaoutengeneza.

Jumamosi, 24 Oktoba 2015

15:13

THABIT ABDUL AANZISHA BENDI MPYA WAZAWA CLASSIC...WAIMBAJI WAPYA WENYE VIPAJI WANATAKIWA.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                       Thabit abdul "mkombozi" mkurugenzi wa bendi ya wakaliwao modern taradance ameanzisha bendi ingine mpya kabisa iitwayo wazawa classic modern taarab katika kuendeleza na kukuza vipaji vya wasanii wachanga wa taarab nchini tanzania.

                Bendi hiyo ambayo tayari imeanza kufanya maonyesho yake katika ukumbi wa cp park night club  uliopo kinondoni manyanya jijini dar kila siku ya jumanne na jumatano inatarajia kuanza kambi hivi karibuni hapa hapa jijini dar katika siku chache zijazo, akiitolea ufafanuzi bendi hii mpya thabit abdul alisema kuwa haitoshirikisha msanii yeyote toka wakaliwao modern taradance, yaani bendi yake mama! isipokuwa itakuwa na wasanii wapya kabisa na ndio maana nasema kuwa huu ni wakati wa wasanii wachanga wenye vipaji kujitokeza na kujaribu bahati yao na atakae fanikiwa kwenye usahili basi moja kwa moja atakuwa ni msanii muimbaji wa bendi hii mpya.

            Nataka kufanya style tofauti kidogo na hii ya taradance ambayo imezoeleka sasa hivi masikioni mwa wapenzi wa taarab, hii wazawa classic modern taarab nataka niifanyie kitu "amazing" ili dunia itambue kuwa mimi ndio mkombozi wa muziki huu wa taarab nchini, nimeandaa usahili kwa wasanii watakaohitaji kujiunga na bendi yangu hii mpya, muda gani, siku gani na wapi nitafanyia usahili nitawatangazia ila kikubwa wanaweza kuwasiliana na viongozi wa wakaliwao na wazawa kwa namba zifuatazo kwa maelezo zaidi nini wanatakiwa kufanya ni:-

 

                                              0787-696731 Thabit abdul

                                              0657-036328 Kais mussa kais

                                              0719-232424 Hashim said

                                              0712-221413 Ally tiketi.

 

           Hizi ni namba za viongozi wa bendi ya wakaliwao modern taradance ambao pia ni viongozi wa wazawa classic modern taraab, yeyote ambae atakuwa tayari kufanyiwa usahili ili aweze kujiunga na bendi hii mpya anaweza kuwasiliana nao kwa maelezo zaidi.

14:26

SENIOR BACHELOR:- SIPO TAYARI KUUNGANISHA BENDI YANGU NA KAPTEN TEMBA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


           Mkurugenzi wa bongo star's modern taarab Senior bachelor amesema yeye hayupo tayari kuunganisha bendi yake hiyo na bendi ya fungakazi chini ya kapten temba kama ambavyo amefanya kanal muhsin kwa kuinganisha bendi yake ya rocky city modern taarab.


MKURUGENZI WA BONGO STAR'S...SENIOR BACHELOR.

          Aliyasema hayo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari hizi kwamba je atakuwa tayari kuunganisha bendi yake ya bongo star's modern taarab na wenzie kapten temba na kanal muhsin?, Senior alisema sioni jipya kwao ambalo litanishawishi mimi kuungana nao! nitabakia mimi kama mimi na wao kama wao ukweli ndio huo! nimefanya kazi na watu hao wote wawili wakati tupo pamoja fungakazi nawafahamu vizuri sana hakuna jipya pale niamini mimi.


         Ikumbukwe kuwa wote hao watatu walikuwa pamoja ndani ya fungakazi modern taarab, Temba akiwa ndio mkurugenzi, senior ni director mkuu wa bendi na kanal muhsin yeye alikuwa ni meneja wa bendi.

Alhamisi, 22 Oktoba 2015

15:28

FUNGAKAZI MODERN TAARAB NA ROCKY CITY MODERN TAARAB ZAUNGANA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


              Bendi mbili za fungakazi modern taarab na rocky city modern taarab wakurugenzi wake wamefikia makubaliano ya kuungana kwa pamoja katika shughuli zao za burudani kwenye kumbi mbalimbali.


FUNGAKAZI MODERN TAARAB.

               Wakizungumza na mwandishi wa habari hii wakurugenzi hao kapten temba na kanal muhsin kwa pamoja wamesema kuwa wamefikia makubaliano hayo ya kuwapa burudani wadau na wapenzi wao kwa pamoja ili kujenga umoja na upendo baina yao, unajua hapo kabla tuliwahi kuwa pamoja katika bendi ya fungakazi modern taarab kanal muhsin akiwa kama meneja ila baadae akaniomba kuanzisha bendi yake ya rock city nami nilimruhusu, na sasa tunaungana tena, kwakweli inapendeza sana alisema kapten temba.


          Nae kanal muhsin kwa upande wake alisema kuwa natambua sana uwezo wa kapten temba katika utunzi na namuheshimu sana hivyo kwa kuungana tena na yeye, mimi binafsi yangu na wasanii wa rocky city  kwa ujumla tumefurahishwa sana. wakifafanua muungano wao walisema kuwa kwa show za kuandaa wenyewe watakuwa pamoja na kushirikiana ila zile show za kununuliwa basi kila bendi itakwenda kivyake labda kama promota akiamua kuwachukuwa kwa pamoja basi watakuwa wote.

Jumanne, 20 Oktoba 2015

19:24

JE UNAWAJUA TAUSI WOMEN TAARAB KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR?...SOMA HABARI KAMILI HAPA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                            TAUSI ni mmoja wa ndege maarufu ambae ni mrembo alieumbika kutokana na umbo lake zuri la kupendeza,uzuri huo pia huonekana kwa manyoya yake ambayo pia ni kivutio kwa wengi wakiwemo watoto wadogo.


Nyimbo mbali mbali ziliwahi kuimbwa ambazo zinaonyesha kumsifia ndege huyo na kuonekana kuvuta mapenzi kwa watu wengi,lakini pia uzuzri wa ndege huyo kumefanya hata kupatikana kwa jina la la mtu kwa uzuri wake.


Lengo langu sio kumsifia wala kumzungumzia ndege huyo ,bali ni kuzuzngumzia mustakabali mzima wa kundi la taarab la akina mama ambalo limeweza kujizolea umaarufu mkubwa sana ndani nan je ya visiwa vya Zanzibar.


Mara baada ya kuona kazi zinazofanywa na akina mama hao mwanzo mwa mwezi huu katika tamasha la Sauti za Busara hamu na shauku kubwa ilinipata ya kutaka kujua kiundani azma na lengo la kuanzishwa kwa kundi hilo.


Niliweza kufika katika Makao Makuu ya Klabu hiyo yalipo katika maeneo ya Kisiwandui mkabala na Msikiti Mabati mjini Unguja na kukutana na Mkurugenzi wa kundi hilo Bi Maryam Hamdani.


Bi Maryam alinielezea tangu kuanzishwa kwake,walipofikia na matumaini ya baadae ya kundi hilo .


Tausi ni kikundi pekee nchini Tanzania kinachopiga muziki wa taarab asilia ambacho kinafanya shughuli zake zote kupitia akina mama wanaoongozwa na Mkurugenzi huyo anaepiga ala ya Qanoon.


Sio jambo la rahisi kuona akina mama hao wanaweza kufanya kazi hasa ya kupiga ala asilia ambazo ni ngumu kutokana na ala hizo kutumika bila ya umeme na ndio jambo lililonifanya niamini kwamba wanawake wakiamua wanaweza.


Jina la Tausi limetokana na Mkurugenzi huyo kumpenda ndege huyo tangu akiwa mdogo na alisema kuwa mapenzi yake yalikuwa kwa ndege wawili ambae ni Tausi na Ziwarde na ndipo akaamua kukiitia kikundi hicho kwa jina la Tausi.


“Tangu utoto wangu Tausi na Ziwarde nilikuwa nawapenda sana nikaamua nikaamua kukiita kikundi hichi jina la ndege huyu na pia nilitaka kubadilisha majina ya vikundi vya taarab na sio kila siku hayo kwa hayo,”alisema Bi Maryam.


Tausi ilizaliwa rasmin Julai mwaka 2009 kikiwa na vijana wa kike 22 ambapo alianza nao kwa kuwafundisha kupiga ala mbali mbali akiwa yeye na walimu wenzake Marehemu Iddi Abdallah Farahan,Mohammed Ilyas,Ramadhan Muhidin na Ali Ibrahim.


Walianza kwa kuwafundisha kutumia ala mbali mbali ikiwemo Qanoon,Udi,Fidla,Violin,Tablah,Key board, Bongos na aina mbali mbali za ala ambazo zinatumika katika muziki wa taarab asilia.


“Hamu yangu ya kupenda muziki wa taarab na mimi mwenyewe nikiwa msanii na pia nafahamu kutumia ala ya Qanoon ndio niaamua kuanzisha kikundi hichi ambapo nilianza na akina mama 22,”alisema.


Mara baada ya kuonekana kwamba upo umuhimu kutokana na kuanzishwa kwa kikundi hicho watu mbali mbali wenye hamu ya kuwa wasanii ambao wanahitaji kujifundisha kutumia ala walianza kujiunga na Tausi.


Mkurugenzi huyo anafahamisha kwamba sharia ya kikundi hicho kuwa hakuna msanii yoyote aliekuwemo ndani ya Tausi lazima ajue kupiga ala na sio kubakia kwenye kuimba tu.


“Wapo wasanii ambao walijiunga na Tausi wakiwa hawajuai chochote zaidi ya kuimba tu,lakini nashukuru kutokana na jitihada ya Tausi na sharia yetu watu wote wajue kupiga ala basi sasa hivi takriban wasanii wetu wote wanajua kutumia ala,”alifahamisha.


Hakuna jambo lizilokuwa na matatizo wala faida,lakini kwa upande wa matatizo yanayokikabili kikundi hicho ni ukosefu wa vifaa ikiwemo kukatika kwa  nyuzi ambazo zinatumika kwenye ala na matatizo mengine amabayo alisemani ya kawaida tu.


Lakini kwa upande wa faida,Tausi imeweza kupata faida mbali mbali ikiwemo kujua kupiga ala,kujiajiri wenyewe kujua zaidi kutumia ala za asili,kupiga taarab katika sehemu mbali mbali na kuweza kusafiri.


Mkurugenzi huyo alizitaja sehemu ambazo wamebahatika kufanya maonyesho ni katika matamasha ya busara kwa miaka mitatu,sherehe za mkutano wa EU sherehe za chakula cha usiku kwa wadau wa elimu pamoja na uzinduzi wa mkutano mkuu wa AU uliofanyika mjini Nairobi na kuhudhuriwa na alikekuwa Makamo wa Rais wan chi hiyo Raila Odinga.


Lakini pia Mkurugenzi huyo alisema kujwa faida nyengine kwa kundi hilo ni kuhudhuria katika matamasha ya kimataifa yaliofanyika nchini Lebanoon na Misri.


“Hii ni faida kwetu na faraja iliyoje kupata kufanya maonyesho katika sehemu mbali mbali tena kubwa ambazi imeweza kutusaidia kukitangaza kikundi chetu pamoja na nchi yetu kwa ujumla,”alieleza.


Aidha kundi hilo pia limeweza kupiga nyimbo mbali mbali pamoja na Bashraf zao wenyewe ambazo zimetungwa katika kundi hilo ambapo miongoni mwa watunzi hao akiwa yeye mwenyewe Mariam Hamdani.


Tausi linatamba na nyimbo zake mbali mbali zikiwemo Usione vyaelea,Walodhani mzaha,Nibembeleze,Si rahisi na dhana ambapo kwa upande wa bashraf zinajuliakana kwa jina la Tausi na Alya.


“Kundi letu limeweza kutunga nyimbo pamoja na bashraf  ambapo tunapokwenda katika maonyesho huwa tunapiga nyimbo zetu wenyewe,”aliongezea Mkurugenzi huyo.


Aidha kwa upande wa matarajio ya kikundi hicho Maryam alisema ni matarajio yao kuwasomesha wasanii wa kundi hilo ndani nan je ya Zanzibar ili waweze kuwa wasanii watakaoitangaza vyema Zanzibar.


“Matarajio yetu Tausi ni kuwapa mafunzo yalio bora wasanii wetu ambayo watayapata ndani nan je ya Zanzibar ili wawe wasanii bora ambao wataitangaza Zanzibar kupitia fani hii ya muziki wa Taarab asilia,”alisema.


Mbali na hayo lakini pia malengo mengine ya Tausi ni kupata wasanii bora wa kike ambao ambao wataweza kutunga mashairi ambayo yatasaidia kuwainua wanawake na pia kutafuta klabu maalum .


Alifahamisha kwamba lengo la kutafuta klabu ni kutaka kuendelea kwa kikundi hicho ambapo alifahamisha kwamba vikundi vingi  sana vya taarab vinakufa kutokana na kukosekana kwa klabu .


Maryam Hamdani ambae pia ni Makamo wa Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)  amewashauri wasanii kuendeleza muziki wa taarab asilia ili waweze kuitangaza nchi yao kupitia fani hiyo.


Pia aliwashauri wanawake kutumia fani hiyo kuwa ni ajira na sio kuifanya fani hiyo kuonekana kuwa ni fani ya kihuni jambo ambalo alisema kuwa sio kweli bali ni dhana potofu kwa watu wasiopenda fani hiyo.


Kutokana na sababu mafanikio hayo,Mkurugenzi wa Tausi ambae pia ni mwanzilishi wa kundi hilo ana kila sifa ya kupewa kutokana na ujasiri wake alionao katika kusaidia kutetea haki za wanawake wenzake katika Nyanja ya muziki wa taarab.


Hii ni faraja kubwa kwa nchi yetu kutokana na mama huyo kuona umuhimu kundi hilo na hakuna budi kwa taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi kukisaidia kikundi hicho ili kiweze kukuwa na kuwapatia ajira akina mama hao.


Tausi ambalo ni kundi maarufu likiwa chini ya mlezi wake aliekuwa Waziri wa Fedha za zamani wa Jamuhuri ya Muungano wam Tanzania Zakia Meghji linaendelea kufanya maonyesho yake katika sehemu mbali mbali za mjini na mashamba... Makala hii ni kwa hisani ya Bin Mahmoud.

Jumamosi, 17 Oktoba 2015

19:39

JE UNAUFAHAMU WIMBO FADHIRA ZA MNYONGE TOKA KWA SAADA NASSOR...PATA KIPANDE HIKI!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                    Anaitwa Saada Nassor muimbaji kutoka Zanzibar one modern Taarab visiwani unguja, umaarufu wake unatokana na sauti yake tamu pamoja na uchezaji wake stejini.

Kwa wanaomfahamu anaitwa "mamaa wa minenguo" hebu pata raha kidogo ya kipande cha wimbo huu.

SAADA NASSOR AKIKABIDHIWA MOJA YA TUZO ZAKE.

Wimbo: Fadhila za Mnyonge

Muimbaji: Saada Nassor mamaa ya minenguo

Moja ya Shairi>>>>>>>>>>>>>>

Kukutendea hisani sikuwa na nia mbaya

Bali ni yangu imani ooooh mwenzangu kusaidia

Wala katu sidhani kwako nina tarajia

Nafahamu huna cha kunifanyia

Usiniweke rohoni na kunipaka ubaya

Kashfa wanifitini mie mshirikina haya

Wema wangu fadhila zangu kwako Mola ndiye anajowa.

malipo yangu yapo kwa Mungu mmiliki wa himaya

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Uvumilvu ni sawa kwani Mola anao

Nastahamili sikujibu yote hayo atayarudi Rabanna

00:52

TETESI:- YOUNG HASSAN ALLY KUTIMKIA MOYO MODERN TAARAB?.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                         Muimbaji wa kutegemewa wa bendi ya ogopa kopa classic inayo ongozwa na malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa, young hassan ally inasemekana yupo katika mazungumzo na uongozi wa moyo modern taarab ili aweze kujiunga nao rasmi.

YOUNG HASSAN ALLY AKIWAPAGAWISHA MASHABIKI WAKE STEJI.

                   Akizungumza na mtandao huu makini Director wa bendi ya moyo modern taarab, mgeni kisoda alisema kuwa ni kweli hizo taarifa lakini kwa sasa wameamua kulisimamisha suala hilo  mpaka uchaguzi mkuu utakapopita hapo october 25, lakini kwa hatua tuliyofikia kwa mazungumzo ya awali sio pabaya!, nae katibu msaidizi wa bendi ya ogopa kopa classic black kopa alipoulizwa na mwandishi alijibu kuwa hana taarifa hizo na wala uongozi mzima wa bendi yao hawajui chochote ila taarifa zitakapowafikia itakuwa hakuna tatizo kwani hassan ally ni msanii kama walivyo wengine kwahiyo ana uhuru wa kwenda bendi yoyote ile na kwa wakati wowote!.Alipopigiwa simu hassan ally mwenyewe simu yake ilikuwa inaita tu bila majibu yoyote.

Alhamisi, 15 Oktoba 2015

13:59

MWENYEKITI WA CHAMA CHA SIASA NLD,NA KIONGOZI WA UKAWA AFARIKI DUNIA LEO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

 

             MWENYEKITI Mwenza wa Ukawa na Mwenyekiti wa chama cha NLD, Emmanuel Makaidi amefariki dunia leo mchana kwa shinikizo la damu akiwa Hospitali ya Nyangao mkoani Lindi.

Wasifu wake

Alizaliwa Aprili 10, 1941 huko wilayani Masasi mkoani Mtwara. Alianza elimu katika Shule ya Msingi Namalenga wilayani Masasi kati ya mwaka 1948 – 1952, mwaka 1953 – 1954 alisoma katika Shule ya Kati (Middle school) iitwayo Luatala hukohuko Masasi.

Baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari ya Chuo cha Mtakatifu Joseph na kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne kati ya mwaka 1953 hadi 1956.

makaidi

Makaidi alisoma darasa la 13 na 14 (kidato cha tano na sita) katika Shule ya Sekondari Luhule, Uganda kati ya mwaka 1957 – 1958. Baada ya hapo alielekea Afrika Kusini na kujiunga na Chuo Kikuu cha Witwatersrand na kuhitimu Shahada ya Uendeshaji na Usimamizi kati ya mwaka 1958 – 1960.

Baada ya kuhitimu vizuri pale Witts, aliendelea kupata ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili, mara hii alielekea Marekani na kusoma masuala ya Menejimenti na Utawala kwa ngazi ya uzamili kati ya mwaka 1960 – 1962.

Alisoma pia katika Chuo Kikuu cha Howard kilichoko jijini Washington, Marekani. Baada ya kurejea nchini akiwa mhitimu wa M.A, Makaidi alianza kazi serikalini mwaka 1966 hadi mwaka 1973 akiwa mchambuzi kazi mkuu, katika kitengo cha Utumishi. Kati ya mwaka 1974 na 1975 (miaka miwili).

Alirudi tena Marekani na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Howard. Aliporejea nchini kwa mara ya pili mwaka 1976 aliendelea na kazi yake pale Utumishi hadi mwaka 1985 alipopewa kazi nyingine kubwa zaidi, akawa Mkurugenzi wa Miundo na Mishahara kwenye kamati iliyokuwa inashughulikia mashirika ya umma nchini.  

Baada ya hapo aliendelea na kazi serikalini ila kuanzia mwaka 1992 hadi mauti yanamfika, Dk Makaidi hajajishughulisha tena na kazi za serikalini wala mashirika binafsi.

Alikuwa amejiajiri akiwa na kampuni kadhaa zilizoajiri Watanzania wa vipato vya kawaida, lakini pia alikuwa akitoa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa kampuni za ndani na nje ya nchi huku akiongoza chama cha NLD akiwa Mwenyekiti.

Dk Makaidi ni mwandishi mzuri wa vitabu, ameshaandika zaidi ya vitabu 10. Marehemu ameacha mke aitwaye Modesta Ponela na walibahatika kupata watoto wanane.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi...Emen!.

00:14

RUKIA RAMADHAN:- SI VYEMA MSANII KUHAMAHAMA...LAKINI PIA MSANII HUHAMA KWA SABABU ZA MSINGI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                “NIKUMBATIE mwenye wivu atazame,Nikumbatie roho yake imuume

Nikumbatie mwenye  wivu alalame,Nikumbatie akujue wangu mume

Njiani nikipita arudi kinyume nyume,Kata kiu yeye Fanta mi sina habari nae

Ajijue cheo chake mina yeye hatufanani,Atuone ashituke anijue mimi nani

Cheza na mimi mpenzi cheza name kwa helenzi,Mambo mazuri laazizi ndo hayataki haraka”

BI RUKIA RAMADHAN.

Ni moja ya beti katika nyimbo maarufu za muziki wa taarab visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wa wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Nikumbatie’ ambao uliimwa katika kundi maarufu la East African Melody.

Maneno hayo ni miongoni mwa wimbo mzima ulioghaniwa na mwanadada mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni sie mwengine bali ni bibie Rukia Ramadhani Ali.

Rukia ni msanii mahiri katika anga la muziki wa taarab ndani nan je ya Tanzania ambae kila kona ya dunia anajulikana kutokana na kipaji chake alichojaaliwa na muumba wake.


Msanii huyo ambae hapendelei kuitwa malkia wa mipasho  kutokana na kutopendelea kuimbwa nyimbo za kupashana na kuelekeza zaidi nguvu zake katika nyimb o za mahaba na kubembeleza.

Nilipomuuliza anajiskiaje kuitwa jina hilo la malkia wa mipasho,hakuonesha bashasha wala haiba yake ya kawaida ya kutabasamu na akajibu ‘sitaki kuitwa malkia wa mipasho kwa sababu siimbi wala sifikirii kuimba mipasho’.

Jibu hilo lilinifanya nishangae kidogo kwa vile nyimbo za mipasho ndio zaidi hivi sasa zinazowapa umaarufu mkubwa  waimbaji wake kiasi cha kumuuliza nini sababu ya msimamo wake huo.

“Mimi ni msanii ninaependa zaidi taarab asilia ambayo lugha ya mashairi yake ni ya kiungwana,haina maneno makali tofauti na taarab ya kisasa,wanaimba tu lakini haina maadili ya Kizanzibari au taarab kwa ujumla,”alisema bila ya kutaka kuingia ndani zaidi.

Nilipotaka kujua alipoanzia hadi alipofikia,Rukia hakukataa tulikwenda hatua kwa hatua hadi mwisho wa mazungumzo yetu,alipoanzia alipofikia na matarajio yake ya baadae.

Msanii huyo alisema alijitosa rasmin katika fani ya muziki mwaka 1974 katikam kikundi cha Tawi la Afro Shirazi Party la Mwembeshauri chini ya mwalimu wake Marehemu Khamis Shehe.

Alisema wakati huo walikusanywa watoto wengi wa mtaani hapo kwa ajili ya kufundishwa masuala ya uimbaji na baada ya mafunzo ya muda walipelekwa majaji wenye uelewa mpana wa muziki huo na uimbaji kwa kuwachuja vijana hao.

Rukia alikuwa miongoni mwa vijanan waliopenya katika mchujo wa majaji hao na hapo ukawa mwanzo wa mafanikio  yake kwa vile kupita huko kulimfanya apelekwe katika klabu maarufu ya tab visiwani humu ya Culture Musical Club yenye maskani yake katika mtaa wa Vuga mjini Unguja.

Alianza mazoezi katika klabu hiyo na hatimae kuanza kuimba akiwa bado mwanafunzi wa shule na hivyo kuweza kubeba majukumu yake yote ya usanii na masomo shuleni.

Alisema alianza rasmin kuanza kupanda jukwaani akiwa na kundi lake la Culture na nyimbo yake ya kwanza ilijulikana kwa jina la ‘Kukupenda sana ndilo kosa langu sitofanya tena naapa kwa Mungu,Nilioyaona yanatosha kwangu’.

Kutoka kwake huko kuliwashtua wazazi wake ambao waliona kwamba anajikita zaidi katika maswala ya nuimbaji,badala ya kuzingatia masomo yake hivyo  ilimsababishia kuhamishwa Zanzibar na kupelekwa  Dar es Salaama kuendelea na masomo.

Msanii huyo mahiri alieleza kwamba alikaa jijini humo kwa muda wa miaka minne na kuendelea na masomo katika shule ya msingi ya Temeke kabla ya kurejea Unguja kuendelea na masomo yake katika shule ya Rahaleo,Kidutani ndogo na kubwa ambapo alimalizia kidato cha nne.


Kurejea kwake Unguja kulimfanya arudie tena kwenye muziki wa taarab na kwa bahati mbaya au nzuri hakurejea tena katika kundi lake la awali bali alihamia kwenye kundi mama la Nadi Ikhwan Safaa.

Alisema akiwa ndani ya kundi hilo,lenye maskani yake katika mtaa wa Kokoni mjini Unguja alikweza kuimba nyimbo kadhaa ambazo ziliweza kumjengea  jina na kumpa umaarufu zaidi.

Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na Nnazama, Nadra na Sadfa,Hidaya, Baada ya dhiki faraja,Niapishe na nyiengine nyingi ambazo zote hizo zinaendelea kupendwa hadi hivi sasa.

Rukia alisema kuanzishwa kwa kundi jipya la taarab la Bwawani ambalo lilikuwa linamilikiwa na hoteli ya Bwawani kulimfanya ahame katika kundi lake hilo na kuhamia katika kundi la Malindi chini ya msanii mahiri Marehemu Mwalimu Abdallah .

Alisema kikundi hicho cha Bwawani hakikudumu muda mrefu sana kwa vile kilivunjika,lakini kabla ya kuvunjika msanii huyo alifanikiwa kukiimbia kikundi hicho nyimbo kadhaa zikiwemo Nidhibiti,na Nadekea change.

Baadhi ya maneno yaliokuwemo katika nyimbo ya Nidhibiti ni kama hivi

Nidhibiti unitunze,Nitunze nihifadhike

Nihifadhi wanyamaze,Nipoe nitononoke

Raha zako nieneze,Milele milele nifarijike

Miti shamba wamalize,Halafu waweweseke.

Rukia ambae ni miongoni mwa wasanii waanzilishi wa kundi la ‘The East African Melody’ ambalo llilianzishwa nchini Dubae mwaka 1992,akiwa na wasanii kadhaa.

Akiwa nchini humo nyimbo za mwanzo alizoimba ni pamoja na Karibu habibi,Nimesharidhika na Nasubiri miujiza na baadae kundi hilo lilihama nchini Dubae na kuhamia visiwani Zanzibar.

Katikati ya mwaka 2000 msanii huyo alipumzika kuimba kwa muda wa mwaka mmoja hadi mwaka 2001 aliporejea tena kwenye ulingo wa taarab na kundi lake hilo la East African Melody.

Mara baada ya kurejea tena msanii huyo alionekana kuendelea kuvutia zaidi  kutokana na kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo zilionekana kuvuta hisia za mashabiki wengi wa muziki wa taarab .

Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na Njoo Habibi,Nani kama wewe,Wastara hasumbuki,Kufa na tai shingoni,Nataka ridhaa yako,pamoja na nyimbo ya Nikumbatie.

Mbali na kuimba Rukia anamudu saana sanaa ya uigizaji ambapo aliwahi kuigiza mchezo wa ‘Mkombozi wa Mwafrika’ambapo alisema kwamba uimbaji uliweza kumletea matatizo kutoka kwa watu mbali mbali ikiwemo kumtishia kumpiga na hata wengine kutaka kumuwekea sumu kwenye chakula.

Pamoja na kutishiwa huko na vitisho hivyo msanii huyo alikabiliana na changamoto hizo ambazo hazikumkatisha tama na kuendelea na shughuli yake hiyo aliyokiri kuipenda ndani ya damu yake.

Rukia hakufafanua kwa nini alitishiwa,lakini alisema hayo ni mambo ya zamani na kwa sasa ayameshapita.

“Kwa kweli nilipokuwa najiunga na mambo ya sanaa nilipata tabu saana kwani nilitishiwa kupigwa na hata kuambiwa nitatiliwa sumu kwenye chakula lakini hayo yalikua mambo ya zamani sasa hivi hayapo,”alisisitiza.

Kuhusu maswala ya faida katika fani ya sanaa,Rukia alisema muziki wa taarab umeweza kumsaidia kupata faida nyingi ikiwemo umaarufu,kuheshimiwa na watu wa rika mbali mbali pamoja na kusafiri.

Alizitaja nchi alizotembelea kupitia muziki wa taarab ni pamoja na Mikoa mbali mbali ya Tanza nia,Kenya,Msumbiji,Comoro,Nigeria,Misri,Dubae,Oman,Abu Dhabi,Jamhuri ya Dominica,Ufaransa,Uswiss,Ubelgiji,Italia,Uholanzi,Slovenia,Ujerumani,Japan,Marekani na Uingereza.

Rukia alisema mpaka sasa kwa yeye ni taarab asilia ambayo ndio mwalimu wake katika fani hiyo lakini pia hiyo haimzuii kuimba taarab ya kisasa.

“Taarab asilia ndio taarab hizi nyengine tunaimba tu kufuata wakati,mimi siwezi kuidharau kwa kuwa ndiko nilipoanzia,”alifahamisha.

Akizungumzia juu ya tabia ya wasanii kuhama hama vikundi mara kwa mara ,alisematabia hiyo sio nzuri ,lakini ijulikane kwamba msanii hawezi kuhama bila ya sababu maalum.

Alijitolea mfano yeye mwenyewe kwamba kuhama kwake hakutokani na maslahi,bali kutokana na matatizo mbali mbali yaliokuwa yakijitokeza.

Msanii huyo hakusita kutoa shukurani zake za dhati kwa wasanii mbali mbali ambao walimuwezesha kudumu katika fani hiyo akiwemo marehemu Asha Simai,marehemu Khamis Shehe na Mohammed ilyas.

Kwa  vile hakuna msanii yoyote ambae hana msanii anaemvutia ,kwa upande wake Rukia alisema anavutiwa na uimbaji wa wasanii wengi akiwemo marehemu Asha Simai,Marehemu Abdulaziz Yussuf na Profesa mohammed Ilyas.

“Marehemu Bi Asha Simai alikuwa akinivutia mno katika fani yake ya uimbaji hasa nyimbo ya iwapi ile ahadi, inanisuuza roho yangu Namuomba Mwenyezi Mungu amsameh makosa yake,”alisema msanii huyo.

Hivi sasa Rukia Ramadhani ni muimbaji huru ambae anaimbia vikundi tofauti anapopata mualiko kikiwemo kikundi cha Zanzibar One Modern Taarab na vikundi vyengine.

Pia msanii huyo ni mwalimu wa sauti(kuimba) katika Chuo cha Muziki wa nchi za Jahazi(DCMA) ambapo aliwataka wasanii kujifunza zaidi  mara wanapoingia katika fani hiyo.

“Nawashauri wasanii kujifunza zaidi kusoma muziki ili waweze kujifahamu na kuelewa nini wanachokifanya jukwaani kwani wasanii wengi hawataki kujifunza.

Rukia Ramadhani Ali ni mtoto pekee wa bwana Ramadhani Ali na Bi Zuhura ambapo mbali na fani ya usanii lakini pia ni muajiriwa wa serikali katika Wizara ya Katiba na Sheria...Makala hii kwa hisani ya Bin Mahmoud.


Jumanne, 13 Oktoba 2015

05:29

MOHAMMED AHMED MOHAMMED GWIJI WA TAARAB ASILIA, UNAIKUMBUKA MAPENZI YANGU POKEA?.

NA KAIS MUSSA KAIS.
  +255657036328

                 “MAPENZI yangu pokea,kwa moyo wa ukunjufu
Wewe nnakulete,usiwe mbabaifu
Kama utayagomea,nitakujua dhaifu”.
Hio ni moja kati ya beti ya wimbo maarufu wa taarab asilia unaojulikana kwa jina la ‘Mapenzi yangu pokea’ulioghaniwa na mutrib mashuhuri na mkongwe ambae ameshastaafu,Maalim Mohammed Ahmed Mohammed.
Bila shaka jina hilo sio geni miongoni mwa wapenzi wa muziki wa taarab asilia wa Zanzibar na hata nje ya visiwa hivi vya marashi ya karafuu.
MOHAMMED AHMED MOHAMMED AKIWA STEJINI.
Licha ya kuwa Mohammed Ahmed ameimba miaka mingi iliyopita,lakini nyimbo zake bado ni dhahabu masikioni mwa wengi kila wanapozisikiliza zikipigwa katika vituo vya  redio au katika rekodi za cd.
Sifa za nguli huyu wa utunzi wa mashairi ya taarab na uimbaji,zilimshawishi mwandishi wa makala haya kumtafuta ili kufanya mahojiano naye,kwa dhamira ya kufahamu tarikh yake katika fani hiyo na siri ya mafanikio yake.
Akisimulia Maalim Mohammed Ahmed alisema fani hiyo hakurithi kutoka kwa mtu yoyote katika familia yake,bali yeye mwenyewe aliipenda pamoja nay eye mwenyewe kuvutwa na ushawishi kutoka kwa wenzake.
Alieleza kuwa mnamo mwaka 1961,ndipo alipojitumbukiza rasmin katika fani ya taarab kwa kujiunga na kikundi cha Nadi Ikhwan Safaa chenye maskani yake katika mtaa wa Kokoni Malindi.
Huko alikutana na wasanii wengi akiwemo marehemu Maalim Iddi Abdallah Farahan,Marehem Maalim Seif Salim,Maalim Abdallah Suleiman na wengine wengi.
Mara baada ya kujitosa kwenye klabu hiyo yenye historia ndefu katika bahari ya muziki wa taarab Afrika Mashariki,msanii huyo amesema alianza kwa kuimba wimbo uliojulikana kwa jina la ‘Wanaodharau mapenzi yafaa tuwaapize’ wimbo ambao hapo awali uliimbwa na mwimbaji mwengine kundini humo.
Baadae alisema akaanza kuimba wimbo ‘Adam na Hawa’ uliotungwa na Marehem Saleh Ajmi ambao alisema hata hivyo wimbo huo haukupata umaarufu kwani uliimbwa mara moja.
Baada ya takriban miaka miwili nyimbo za kukopia na zilizotungwa na watunzi wengine,Maalim Mohammed Ahmed alisema mwaka 1963 alianza kutunga na wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni ‘Mapenzi yangu pokea’ ambao mpaka sasa bado unapendwa.
Kuanzia hapo kasi yake ya utunzi ikapamba moto ambapo zipo nyimbo alizotunga na kuimba mwenyewe na nyengine zikaimbwa na wasanii wengine katika kundi lake hilo.
Baadhi ya nyimbo hizo ni ‘Ua’  ulioimba na Almarhum Maalim Seif Salim ‘Kisebusebu’,Almarhum Bakari Abeid ‘Kibiriti na Petroli’ Maalim Seif Salim,pamoja na ‘Sasa sinae’ulioghaniwa na Almarhum Khamis Shehe.\
Mnamo mwaka 1964 wakati vikundi vyote vya Unguja vilipoungana na kuunda kikundi kimoja cha Mila na Utamaduni,Mutrib huyu alikuwa miongoni mwa wasanii waliojumuika kuanzisha kikundi hicho ingawa baadae aliondoka na kwenda masomoni.
Lakini baada ya kurudi kutoka masomoni,alieleza kuwa uongozi wa klabu ya Culture ulimuomba ajiunge nao na kumpa wadhifa wa Ukatibu,ingawa halikumzuia kuendelea na Nadi Ikhwan Safaa.
Wakati nikizungumza na gwiji huyu alinambia ametunga nyimbo nyingi sana,lakini nyengine amezisahau .
Hata hivyo,aliutaja mmoja wa wimbo alioutunga ambao aliupa jina la ‘Kunguru’ ambapo alinambia aliutunga na kuuimba yeye mwenyewe.
Baadhi ya maneno yaliokuwemo katika wimbo huo ni kama yafuatayo:
Kunguru ndege laghai,Anatabu kumnasa
Kama yeye hatokei,Mwenye hila na mikasa
Japo ukifanya rai,Weka mbele kumkosa.
Aidha Maalim Mohammed Ahmed alibainisha kuwa,hata klabu ya Culture yenye maskani yake mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar,aliitungua nyimbo kadhaa zikiwemo ‘Pesa’ ambao uliimbwa na msanii mkongwe Nihfadhi Abdullah, ‘Kukupenda sana ‘Rukia Ramadhan’  Sikujua kama mapenzi matamu nao ulighaniwa na bibie Mtumwa Mbarouk
Wimbo wa sikujua kama mapenzi matamu ulikuwa ukisema kama hivi:
“Ni hakika sikujua kwamba, Mapenzi matamu
Si dhihaka nakwambia,Yatanitia wazimu
Hivi sasa natambua,Kwamba yamenilazimu
Kila nikiliridhia,Inazidi yangu hamu.

Mbali na wimbo huo pia alitunga wimbo Pendo letu lishasibu  ambao uliimbwa na mkongwe mwengine na mwalimu katika jukwaa la sanaa za maigizo na tarab asilia Marehemu Bakari Abeid Ali.
Muziki wa taarab umeweza kumfikisha mkongwe huyo katika nchi mbali mbali duniani.
Alizitaja nchi hizo kuwa ni Kenya,Visiwa vya Comoro,Dubai na Abudhabi,Oman,Hispania,Ubelgiji,Ufaransa,Uholanzi,Italia,Denmark,Uswisi,Finland,Visiwa vya Reuniuon na nyenginezo.
Pia ametembela Mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara ambapo alikwenda kutumbuiza na klabu zake kwa vipindi tofauti.
Nilipomuliza anifafanulie tofauti anazoziona baina ya taarab asilia na ile inayoitwa ya kisasa,Maalim huyo kitaaluma,kwa sasa hakuna watunzi wa maana bali waliopo ni watu wanaotafuta maslahi pekee bila ya kuzingatia maadili na mambo muhimu katika utunzi wa nyimbo za taarab.

Alifahamisha kwamba wakati yeye anajiunga na taarab,ilikuwa lazima mtu alipie shilingi kumi na baadae kila mwezi shilingi tatu kinyume na miaka hii ambapo msanii anajiunga katika kikundi kwa matarajio ya kulipwa kabla hajaanza kutoa mchango wowote kukiinua kikundi anachojiunga nacho.

“Kuna tofauti kubwa kati yetu wasanii wa zamani na hawa wasanii wa sasa,sisi tulikujwa hatulipwi bali tukilipia ada ya klabu,mimi mwenyewe  wakati najiunga nililipa shilingi kumi na kila mwezi wanachama sote tulikuwa tunalipa,leo wasanii wanalipwa wao” alisema.
Kuhusu tofauti ya kimuziki,Maalim alisema hakuna kitu kinachoitwa modern taarab,bali hiyo ni aina ya ngoma iliyoingia mjini na kwa kuwa kiingiacho mjini si haramu  basi mambo yanakwenda tu kama yanavyoonekana.

“Taarab lazima ipigwe kwa kutumia ala za asili kama vile qanoon,oud,fidla na nyenginezo,lakini leo mtu unaweza kuwa na keyboard  yako ukapiga taarab,mimi sijawahi kuona kama wenzetu Tanga wanaita kumbwaya na Mombasa wanaita Chakacha basi  na hapa kwetu Unguja watafute jina lakini sio taarab,”alifafanua.

Nilitaka pia kujua ni wasanii gani wanaomvutia katika kazi zao,naye bila ya kigugumizi akawataja baadhi ya wasanii akiwemo Marehemu Rashid Sultan,Marehemu Bakari Abeid,Marehemu Seif Salim,Ali Soud na Marehemu Maulid Mohammed Machaprala.

Hata hivyo,kwa maneno yake,alieleza kuwa miongoni mwa wanawe hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kama anafuata nyayo zake za usanii,ingawa alimtaja mmoja wa watoto wake aitwae Harusi kuwa anaonekana kujaribu kutaka kujiingiza katika tasnia hiyo..
Nilipomtaka atoe maoni juu ya dhana ya baadhi ya watu kuwa muziki ni uhuni,Maalim Mohammed alikuwa na fikra nyengine tofauti na kusema kuwa uhuni ni tabia ya mtu kwani wapo wahuni wanaojulikana sana katika jamii lakini kamwe hawafanyi kazi ya muziki wala usanii wa aina yoyote.

“Hizi ni dhana potofu muziki ni kazi kama kazi nyengine zinazoweza kumjengea mtu heshima na kutambulika kitaifa na kimataifa,pia muziki umetumika katika kusaidia mambo mbali mbali kwani una nguvu ya kuhamasisha.

Na zaidi mbona mimi sijawa muhuni,Umkulthum,Abdelhalim Hafidh na wengine wengin hawajakuwa wahuni,”alitoa mfano.

Juu ya siku hizi kutokuwepo kwa watunzi wengi wa masihairi ya taarab,msanii huyo alisema hiyo inasababishwa na muziki kugeuzwa biashara ,ambapo alisema watunzi wa sasa wanataka kulipwa na walipaji hakuna .

Akitoa mfano wa klabu za Malindi na Culture ambazo alisema zinashindwa kutoa nyimbo mpya kutokana na kushindwa kulipia.

Mbali na fani ya muziki,lakini msanii huyo aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali Serikalini baada ya awali kuwa mwalimu mkuu katika skuli tofauti ikiwemo Langoni, Wilaya ya Magharibi mwaka 1971,Ole(1972) Kisiwandui(1974) na baadae mwalimu mkuu skuli ya Sekondari Shangani mjini Unguja.

Aidha aliwahi kuwa Afisa wa Mambo ya Kale,Mkurugenzi Mipango Wizara ya mila na Utamaduni,Katibu Muhtasi Ikulu Zanzibar,Katibu Muhtasi wa Rais Ali Hassan Mwinyi Zanzibar,na Baadae Katibu Mkuu Afisi ya Rais.

Nafasi hiyo ya Katibu Mkuu alianzia kipindi cha Rais Marehemu Idrissa Abdulwakil na kuendelea mpaka wakati wa Rais Dr Salmin Amour Juma alipomaliza muda wake nae akafikia muda wa kustaafu.

Kupitia makala hii Maalim Mohammed Ahmed amewashauri wasanii wasikimbilie kuimba tu bali wajifunze kwanza apamoja na kutafuta ujuzi wa kupia ala mbali mbali za muziki wa taarab.

Alitoa mfano wa kikundi cha taarab asilia kinachoundwa na wanawake watupu cha Tausi ambacho kinawafundisha wasanii wake kuimba pamoja na upigaji wa ala.

Pia aliwaasa wasanii kuacha tabia ya kupikiana majungu na fitina katika vikundi ili kuepusha kuvunjika kwa vikundi hivyo.

Msanii huyo aliyebaki kuwa miongoni mwa mifano ya kuigwa alizaliwa mwaka 1940 katika mtaa wa Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja akiwa motto wa kwanza katika familia ya watoto watano wawili wakiume na watatu wakike.

Alianza kupata elimu ya msingi mwaka 1946 katika skuli ya ambayo wakati huo ikiitwa Mnazi Mmoja kuanzia darasa la kwanza hadi la pili ambapo skuli hiyo hivi sasa imekuwa kituo cha American Corner.

Baadae alihamia skuli ya Gulioni huko alisoma mpaka darasa la sita na kuhamia Kiembesamaki kwa masomo ya darasa la saba na la nane kabla ya kujiunga na ‘Junior Secondary School’ ambayo kwa sasa ni Benbella kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tatu.

Mnamo mwaka 1961 alijiunga na Chuo cha Ualimu na kuanza kusomesha mwaka 1962.

Ilipofika mwaka 1976 alijiunga na elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ngazi ya ‘Bachelor of Education’ na kumaliza mwaka 1979.
Mwaka 1983 alikwenda nchini Uholanzi kuendelea na masomo yay a digrii ya juu (Masters).

Gwiji huyo ameoa na amejaaliwa kupata watoto na pamoja na kustaafu taarab,amesema hupata wasaa wa kujikumbusha kuimba hususan katika shughuli maaalum ikiwemo harusi za familia yake... Makala hii kwa hisani ya Bin Mahmoud.