TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 23 Novemba 2015

OMARY KISILA PRODUCER BORA ASIE NA MAJIVUNO, MPAKA SASA AMESAIDIA VIJANA WENGI KATIKA STUDIO YAKE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                   Unapozungumzia ma-producer bora wa muziki wa taarab hapa nchini kwa sasa basi jina la omary kisila ni lazima ulitaje, alianza kama masihara kupiga kinanda kwakuwa ana hobby, amepitia bendi kadhaa mpaka hapa alipo.

OMARY KISILA AKIWA KATIKA STUDIO YAKE MTONI MTONGANI JIJINI DAR.

 

            Omary kisila kwa sasa ana studio yake mwenyewe ya kurekodi muziki iliyopo mtoni mtongani jijini dar na ameshafanya recoding nyimbo kadhaa wa kadhaa mfano Expire date, cheo ni dhamana, kunyamaza si ujinga za rocky city modern taarab, funga domo na fisadi kafilisika za bongo star's modern taarab, Sibadili nia yangu na hata nawe uniseme mie za fungakazi modern taarab, Sielewi kosa langu, thamani ya pendo ni ndoa za wakaliwa town modern taarab na nyimbo nyingine zipo namalizia mixing si vyema nikazitaja pasipo ruhsa ya wamiliki wenyewe.vile vile narekodi aina mbalimbali za muziki mfano kwaya, bongo freva, mnanda au mchiriku, kaswida ambazo zingine zipo redioni zinachezwa. yeyote atakaetaka  mawasiliano ya producer huyu basi atumie namba zake za simu zifuatazo:- 0714-873600.

OMARY KISILA AKIWA STUDIO.

 

            Ikumbukwe omary kisila ndio director wa tanzania motto modern taarab "t motto" inayoongozwa nae mpambanaji Amin salmin, kwa sasa bendi hiyo imekuwa kimya sana lakini tunawaahidi wasomaji wetu kuwa tutamtafuta mkurugenzi huyo azungumze nini sababu ya ukimya wao huu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni