TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 30 Novemba 2015

USIKOSE UTAMBULISHO WA VIJUKUU WA TEGO NA NYIMBO MPYA ZA COAST MODERN TAARAB TAREHE 9/12/2015.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                 Wale watoto ambao kwa sasa ni gumzo mjini, vijukuu wa tego wanataji kufanya onyesho la nguvu katika utambulisho wao sambamba na nyimbo mpya za coast modern taarab siku ya jumatano tarehe 9/12/2015 pale katika ukumbi wa ikweta grill mtoni kwa azizi ally jijini dar.


            Akizungumza na mtandao huu mratibu wa onyesho hilo na ambae ni meneja wa watoto hao yusuph tego alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na bendi tulizozialika na zitatumbuiza sambamba na vijukuu hawa nazo ni dar modern, msondo ngoma, khadija kopa, msagasumu na jokha kassim, pia bendi ya coast modern taarab itatambulisha nyimbo zao mpya kabisa ambazo hazijapelekwa redioni, kwa mara ya kwanza zitasikika pale ikweta grill mtoni kwa azizi ally.


           Show inarajia kuanza saa 1 kamili jioni mpaka majogoo na kiingilio itakuwa ni shilingi elfu tano tu mlangoni, ma-mc wa shughuli hiyo ni sakina lyoka wa cloud's redio na televisheni na mariam migomba wa tbc fm na tbc televisheni. wadau mnaombwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani kutakuwa na ma-surprise kibao na bendi zote zimejiandaa vya kutosha kuwaletea burudani ya nguvu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni