Na pambe za taarab.
Wiki chache baada ya iliyokuwa washawasha classic modern taarab kusambaratika, habari za udukuzi kutoka katika vyanzo vyetu vya habari inasema imezaliwa bendi iitwayo halichachi classic modern taarab ambayo ipo chini ya mkurugenzi Amour magulu pichani.
Habari zaidi zinasema kwamba bendi hiyo tayari imeanza kufanya maonyesho yake katika kumbi mbalimbali tokea sikukuu ya Idd. mtandao huu ulijitahidi kumtafuta mkurugenzi wa bendi hiyo mpya mr amour magulu ili aweze kuwathibitishia wapenzi wa taarab nchini lakini simu yake iliita pasipo kupokelewa, lakini tunawaahidi kuendelea kumtafuta mpaka tutakapompata ili aweze kulizungumzia hili.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni