Na pambe za taarab
Muimbaji wa bendi ya yah tmk modern taarab ambae hapo kabla alikuwa katika bendi ya supershine modern taarab Baby ruby amewashukuru viongozi na wasanii wote wa bendi yake hiyo mpya kwa ushirikiano mkubwa waliomuonyesha kwa kipindi kifupi alichojiunga nao.
Baby aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano na mtandao huu kwa njia ya simu baada ya kuulizwa anaonaje ushirikiano uliopo yah tmk akilinganisha na supershine ambapo alikuwepo mwanzoni?, unajua supershine sikuwa na changamoto za uimbaji tofauti na hapa yah tmk! huku kuna ushindani mkubwa maana waimbaji karibia wote wana viwango vikubwa na wanatambulika sana katika tasnia hii ya taarab nchini, hapa nilipo naona nimeongezeka kiwango kwa asilimia kubwa mno ukilinganisha na nilipokuwa pale supershine.
Kwa sasa hapa yah tmk nina wimbo mpya nimekabidhiwa ambao tutaanza kuufanyia mazoezi mwanzoni kabisa mwa mwaka mpya 2018 jina la wimbo huo siwezi kutaja kwa sasa ila wapenzi na mashabiki zangu nawaomba waendelee kuvuta subira kwani mambo mazuri yanakuja kutoka kwangu alizungumza kwa kujigamba msanii huyo mpole na asie na majivuno.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni