TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 18 Januari 2018

KAPTEN TEMBA ABARIKI ZAINAB MACHUPA KUONDOKA FUNGAKAZI MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab.

Mkurugenzi wa fungakazi modern taarab ambae pia ni mume wa halali kabisa wa zainab machupa, ndugu Kapten temba amezungumza na mtandao huu na kusema amembariki mkewe kuondoka fungakazi modern taarab na kujiunga na yah tmk modern taarab.

Ndugu mwandishi, mimi ndio mume wa Zainab machupa na taarifa za yeye kujiunga na bendi ya yah tmk nilikuwa nazijuwa vizuri tu na nazungumza kwa moyo mmoja kwamba nimemruhu mke wangu kufanya kazi na bendi yake hiyo mpya. Mbona omary tego anaimbia yah tmk na mkewe anaimbia coast modern taarab alihoji mkurugenzi huyo.

Mimi napenda niwatoe wasiwasi viongozi wa yah tmk kuwa hakuna jambo lolote ambalo naweza kufanya katika kumkataza mke wangu kuimbia bendi hiyo, na hata kama watanihitaji kumuwekea sauti Zainab machupa katika wimbo mpya ambao watampatia basi mimi nipo tayari kushirikiana nao kwani naamini mimi namjua sana Zainab hususani katika uimbaji wake ni shairi la aina gani linamfaa, namtakia mafanikio mke wangu katika maisha mapya ya sanaa akiwa na bendi yake hiyo mpya alimaliza kwa kusema Kapten temba.

Ikumbukwe Kapten temba ni mkurugenzi wa bendi ya fungakazi modern taarab ambayo Zainab machupa alikuwa akiimbia huko, mtandao huu unampongeza Kapten temba kwa kuonyesha uungwana wa dhati kabisa kumruhusu mkewe kufanyakazi nje ya bendi yake, ni wanaume wachache sana wenye uelewa mkubwa kama yeye.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni