TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 23 Machi 2016

JAMALI MPERAMPERA:- NIPO KATIKA MAZUNGUMZO NA WASANII WATATU TOKA BENDI KUBWA HAPA JIJINI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Mkurugenzi wa aljazeera modern taarab Jamali mperampera amejinasibu kwamba katika kuendelea kuiboresha zaidi bendi yake yupo katika mazungumzo na wasanii watatu tegemezi na muhimu huko watokako, nia ni kusuka kikosi bora na cha ushindani.
MKURUGENZI WA ALJAZEERA JAMALI MPERAMPERA.


     Aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano na mtandao huu hususani pale alipoulizwa swali la kizushi kwamba ana uwezo wa kuchukuwa wasanii wengine wazuri kama ilivyokuwa kwa Hamisi chizi? au ndio ameishia pale tu?, ndugu mwandishi napenda nikwambie jambo moja...mimi ndio jamali mperampera waulize wakali wa mji huu wananijua vizuri, mara nyingi huwa sishindwi na jambo lolote lile ambalo nakuwa nimeliamulia!, naweza kuchukuwa mpaka bendi nzima nini msanii mmoja? alihoji jamali mperampera huku akisisitiza.


       Nazishauri bendi zingine zinazopiga old is gold kama sisi kwamba wajiandae kupoteza wasanii wao wanao wategemea kwani bado nipo katika kusuka zaidi bendi yangu kabla ya safari ya falme za kiarabu mwezi wa tano mwaka huu, nataka wasanii watatu wakali na mpaka sasa nipo katika mazungumzo na wasanii hao, kwa kukudokeza tu wanatokea katika bendi inayofahamika tu hapa mjini nisingependa kuitaja jina kwani ni mapema sana, nataka bendi iwe namba moja kwa kila nyanja hapa jijini hususani katika hii taarab yetu asilia alisema mkurugenzi huyo.


      Katika siku za karibuni bendi hii ya aljazeera modern taarab imekuwa katika msuguano mkali sana na gusagusa min bendi haswa pale walipomchukua mpigaji kinanda wa bendi hiyo Hamisi chizi, wadau na wapenzi wa mtandao huu hebu tusubiri kuona ni wasanii gani hao ambao wanatarajia kujinga na aljazeera modern taarab? na wanatokea bendi gani? tuvute subira.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni