NA KAIS MUSSA KAIS
Nini ni chimbuko haswa la muziki wa taarab katika afrika mashariki na kati?, hususani katika nchi ya tanzania na ukanda wa pwani kwa ujumla?.
 |
KIKUNDI CHA CULTURE MUSIC CLUB. |
Taarab
ina historia ndefu katika muziki wa Tanzania kama ulivyokuwa muziki wa
dansi. Wapenzi wa taarbu wa zamani waliiweka taarabu katika vyanzo kama
Taarab ya Tanga, Taarab ya Dar es Salaam,Taarab ya Zanzibar na Taarab ya
Mombasa. Taarab ya Zanzibar wakati huo ilikuwa ni ile yenye kundi kubwa
la wanamuziki, kwa kufuata mfumo wa muziki huo kama ulivyokuwa ukipigwa
huko Misri. Historia inatueleza kuwa Sultan Sayyid Barghash wa
Zanzibar kwenye mwaka 1870, alipeleka wanamuziki wake wawili kwenda
Misri kupata taaluma ya upigaji wa Taarab , na waliporudi ndipo mwaka
1905 wakaanzisha klab ya Ikwaan Safaa, kundi ambalo pamoja na kupitia
misukosuko mingi ya kisanii na hata kisiasa, lipo mpaka leo. Na muziki
wa kundi hili na makundi mengine yalifuata aina hii ya muziki kwa muda
mrefu, ulikuwa unajumuisha kundi kubwa la wanamuziki wenye vifaa
mbalimbali kitaalam wanaweza kuitwa orchestra. Taarab ya Dar es Salaam
haikupishana sana na ile ya Zanzibar wakati huo, hapa Dar kukiwa na
vikundi kama Egyptian Musical Club na Alwatan Musical Club vilivyoanza
tangu kwenye miaka ya 30. Mombasa ilijulikana sana kwa aina yake ya
Taarab iliyofanywa maarufu na akina Juma Bhalo waliokuja na upigaji
ulioiga mipigo ya muziki wa kihindi, uliopata umaarifi kutokana na
sinema za kihindi. Ukisikiliza nyimbo maarufu za Juma Bhalo kama Pete,
utasikia uimbaji upigaji na upangaji zauti unaofanana sana na muziki wa
kihindi. Taarab ya Tanga kwa kweli ndio ilistahili kuitwa modern taarab,
taarab hii ndio ilikuwa ya kwanza kuanza kuingiza vifaa ambavyo
vilikuwa vigeni katika taarabu, magitaa, akodian , na mipigo ya ngoma za
kiasili, na pia vikundi vya Tanga vilikuwa vidogo vikiwa na washirika
wa wastani wa watu kumi na mbili. Kazi za Black Star na Lucky Star wengi
tunazijua na waimbaji wake maarufu kama Bi Shakila, Hasmahani sauti zao
zilitawala anga ya muziki huu katika miaka ya sabini..
 |
BI SIHABA JUMA AKIBURUDISHA WAPENZI WAKE WA TAARAB ASILI. |
Katika
anga za leo kuna vikundi vingi vinavyotangaza vinapiga muziki wa
taarabu, jambo ambalo limepingwa na wengi kuwa kinachopigwa pigwa sasa
si taarabu, kuna hata waliofikia kusema kwa vyovyote vile kinachoitwa
mipasho hakina uhusiano wowote na taarab!!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni