Mengi yalisemwa pale muimbaji maarufu wa bendi ya Jahazi Modern Taarab AMIGO alipokuwa kasimamishwa kuendelea kufanya kazi na bendi yake hiyo kwa utovu wa nidhamu kwa viongozi wake.Lakini kwa busara na hekima alizonazo kijana huyu alinyamaza kimya wala hakuwa mtu wakuzungumza sana na vyombo vya habari mpaka pale alipozungumza kwa mara ya kwanza na mtandao makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com na kukili makosa yake pia kuuomba uongozi umsamehe kwa kosa alilokosa.
AMIGO AKIWAJIBIKA STEJI. |
Amigo alithibitisha hayo pale nilipokutana nae katika show ya bendi ya Supershine Modern Taarab alikuja kutembea ambapo bendi hiyo ilikuwa inafanya onyesho lake katika ukumbi wa Mirambo Annex Buguruni siku ya jumatano, alianza kwa kusema kwanza kabisa namshukuru mungu kwa kunipa hekima,busara na khali ya kujitambua na utii uliotukuka mpaka kugundua makosa yangu, pili napenda niwashukuru viongozi wangu kwa kunisamehe na kunirudisha tena kazini.
AMIGO AKIFANYA MAHOJIANO REDIO. |
Tatu napenda kuwashukuru wale wote ambao nilikuwa nao bega wa bega kipindi chote cha matatizo yangu wakinipa ushauri mzuri na wenye busara mpaka kufikia hapa, vile vile mke wangu Mama Man! amefanya kazi kubwa sana kunirudisha katika hali ya kawaida ahsante sana mke wangu nakupenda sana tuu!.
Dawati la ubuyuwataarabutz.blogspot.com kwa pamoja tunapenda kuupongeza uongozi wa bendi ya Jahazi Modern Taarab kwa kuweza kufikia maamuzi ya kumsamehe kijana wao na kumrudisha tena kundini...big up kwenu!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni