Muimbaji wa Dar Modern Taarab, Hassan Vocha yupo katika hatihati ya kukosa kushiriki Tamasha kubwa la Mitikisiko ya Pwani ambalo limepangwa kufanyika siku ya kesho jumamosi tarehe 13/12/2014 katika ukumbi wa Dar Live uliopo mbagala jijini Dar!.
![]() |
HASSAN VOCHA MUIMBAJI WA DAR MODERN TAARAB. |
Mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com ulifuatilia habari hii kwa makini na uhakika zaidi kama ilivyo kawaida yake, na kuweza kuzungumza na Hassan mwenyewe siku ya jana alhamisi maeneo ya nyumbani kwake mwembe yanga Dar, Nilianza kwa kumpa pole kwa tatizo lililompata na kumuuliza ilikuwaje mpaka akafikia kuanguka?. Alianza kwa kusema kwanza kabisa namshukuru mungu kwa kuweza hata kuzungumza na wewe hivi! kiukweli hali haikuwa nzuri na tatizo lilikuwa kubwa sana.
HASSAN VOCHA |
![]() |
HASSAN VOCHA AKIFANYA MAHOJIANO NA MARY BOSSA!. |
Mimi kipaji kanipa mungu na hakuna wakuitoa roho yangu zaidi ya mungu, hao wanaotaka kuishusha nyota yangu wanajisumbua kwani wanapoteza muda wao na wala katu hawatofanikiwa. kwa sasa naendelea vyema namshukuru mungu ila bado sijajua kama nitaweza kuimba hapo kesho pale Dar Live mbagala au lah!.
Hali ya kiafya ya Hassan Vocha inaendelea vizuri kwani anatumia dawa pamoja na maduwa anayosomewa na Ostaadh wake, mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com unampa pole Hassan Vocha kwa maradhi yaliyo mfika na inshallah mwenyezimungu atamjaalia atapona haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni