NA KAIS MUSSA KAIS
Coast Modern Taarab ni bendi yenye historia kubwa katika kuleta mapinduzi ya muziki huu kulingana na wakati tulionao kwa sasa, siku za hivi karibuni bendi hii imekuwa kimya sana, lakini unapozungumza na mkurugenzi wa bendi hii Omary Tego hatosita kukuambia wanajipanga kwanza katika kulisoma soko la muziki huu linahitaji radha ya namna gani!.
 |
MAUA TEGO AKIFANYA YAKE!. |
Maua Tego ambae ni Dada wa Omary Tego ndio kinara wa kundi hilo na kwa sasa yupo katika maandalizi makubwa ya kutoa wimbo mpya kabisa uitwao "Mume ni bonge la issue" mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili au mwanzoni mwa mwezi wa kwanza wapenzi wategemee kuusikia wimbo huo hewani. Akizungumza na mtandao huu Mau Tego alisema wimbo huu ni mzuri sana na ana matumaini makubwa kwamba utarudisha ile hadhi ya Coast Modern Taarab ambayo imekuwa ikipotea kila kukicha.
 |
MAUA TEGO NDANI YA DAR LIVE!. |
Kwa upande wa Mkurugenzi Omary Tego yeye amesema anashukuru kuona timu yake ipo kamili na amejipanga kurudi katika nafasi yake kama kawaida, wimbo huu wa Maua tunatarajia kuurekodi hivi karibuni sababu tumesha ufanyia mazoezi vya kutosha na kila kitu kipo sawa, kikubwa nawaomba wapenzi waendelee kutupa sapoti nasi tunawaahidi hatutowaangusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni