TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 13 Desemba 2014

MITIKISIKO YA PWANI:- NANI ZAIDI LEO...HASSAN ALLY NA OGOPA KOPA AU PRINCE AMIGO NA JAHAZI?.

NA KAIS MUSSA KAIS

            Ule mpambano uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu kubwa kati ya vijana wawili wenye uwezo sawa kimtazamo, hapa namzungumzia Prince Amigo "Kirikuu" au mtoto wa mfalme akiwa na Jahazi Modern Taarab na Young Hassan Ally "Mr pendwapendwa" akiwa na kundi zima la Ogopa Kopa Classic Bend, leo ndio leo pale katika ukumbi wa Dar Live mbagala jijini Dar watakapopanda katika jukwaa moja kila mmoja kwa muda wake kuudhihilishia umma wa watanzania kwamba yeye ni zaidi ya mwengine!.

         Vijana hawa ambao wamekuwa wakifanya vizuri sana katika bendi zao na hata wapenzi na mashabiki zao wamekuwa wakirumbana kutaka kujua  nani ni mkali baina yao? Ushindani uliopo baina ya vijana hawa

YOUNG HASSAN ALLY MUIMBAJI WA OGOPA KOPA CLASSIC BENDI.
ni mkubwa kwa sasa mpaka umepelekea watu kupigana kwa ajili ya kubishania uwezo wao wanapokuwa stejini, Hassan Ally anacheza sana pindi anapokuwa anaimba na hata Prince Amigo nae anacheza sana tu, sasa hapa ndipo kwenye utata mkubwa kimaamuzi, kwenye kuimba pia wote wanafanya vizuri...yaani huu ni mpambano utakao amua nani mkali.

         Kwa upande wa Amigo yeye anasema Hassan Ally ni mtoto mdogo kwake kisanaa na leo atahakikisha anampoteza kabisa katika steji, najiamini kwa kazi yangu ninapokuwa steji, nawaomba wapenzi wangu wajitokeze kwa wingi ili washuhudie nitakavyo muacha mbali huyu jamaa. Yeye Hassan Ally anasema kwamba hizo anazotoa huyo mtoto Amigo ni kelele za Chura hazimzuwii tembo kunywa maji, mimi ndio Young Hassan Ally mara zote na siku zote nimezaliwa kushinda! simuogopi huyo dogo Amigo, mimi nashindana na mfalme sio yeye hana jipya kwangu na wala simuhofii! nitampoteza kabisa leo pale stejini wadau njoeni muone atakavyo tapatapa, mimi ndio kabali yao hapa mujini bhanaa!.

PRINCE AMIGO WA JAHAZI MODERN TAARAB.
       Sisi kama wadau wakubwa wa Taarab nchini tutakuwepo ukumbini kuchukuwa matukio kadhaa wa kadhaa ili kuwahabalisha wasomaji wetu nini kimejili na nani kakalishwa baina yao.Stay tune!.

       

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni