TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 14 Desemba 2014

MITIKISIKO YA PWANI 2014:-WAKALIWAO MODERN TARADANCE WAJIONDOA HATUA ZA MWISHO...WAPENZI WAPIGWA NA BUTWAA!!.

NA KAIS MUSSA KAIS

              Tamasha la mitikisiko ya pwani lilifanyika usiku wa jana katika ukumbi wa Dar Live mbagala jijini Dar na kushuhudia bendi ya Wakaliwao Modern Taradance wakigoma kabisa kupanda stejini, katika hali ya sintofahamu tatizo lilianza pale ilipotakiwa bendi moja wapo kati ya Dar Modern au Wakaliwao ianze kufungua utepe wa tamasha hilo kubwa afrika mashariki na kati.

THABIT ABDUL "THE DON".
        Mabishano makubwa yalizuka kila bendi ikigomea kuanza, ndipo busara zaidi ilipotumika na wasanii wa Dar Modern kupanda stejini na kuanza onyesho hilo. waliposhuka Dar Modern wakapanda East African Melody akafuatia msagasumu kabali yao, wakaja Mashauzi Classic, Jahazi Modern Taarab mwisho kabisa wakamalizia Ogopa Kopa.

        Katika khali ya kushangaza alisikika Mc Didda akitangaza kwamba wakaliwao wamepatwa na udhuru kwahiyo pamoja na kwamba wamefika humu ndani lakini hatutokuwa nao! ina maana hawatopanda stejini!, watu walianza kunung'unika na maneno mengi yalisemwa, uchunguzi wa awali uliofanywa na mtandao huu unaonyesha kwamba Thabit Abdul sambamba na bendi yake ya Wakaliwao Modern Taradance

THABIT ABDUL NDANI YA POZI.
walikuwa wanalalama kuhujumiwa na waandaaji wa Tamasha hilo kwa kupendelea baadhi ya bendi flani.

       Tulipomtafuta mkurugenzi Thabit Abdul azungumzie hili hakupatikana katika simu yake, ila tunapenda kuwaahidi wapenzi na wasomaji wa mtandao huu makini kwamba tutawaletea habari hii kwa kina zaidi baada ya kumpata Thabit Abdul na kueleza ni kwanini bendi yake haikuweza kupanda stejini wakati ilishatia timu ktk ukumbi huo?.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni