Onyesho hili linaweza kuwa ni onyesho litakalobeba hisia za watu wengi sana ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kwani linajumuisha magwiji wa muziki tofauti ambao wanatamba hapa Afrika Mashariki kwa kipindi hiki, namzungumzia Mfalme Mzee Yusuph na Diamond Platnum au ukipenda muite "kabali ya tuzo Afrika kwa sasa".
![]() |
HAWA NI WAFALME WAWILI BALAAH!. |
Mzee Yusuph ndio msanii au muimbaji wa muziki wa Taarab mwenye mafanikio kuliko waimbaji wote katika muziki huo kwa sasa, amefanikiwa kupata tuzo nyingi kuliko wote na bendi yake ya Jahazi Modern Taarab ni bendi yenye mafanikio makubwa kuliko bendi zote habari ndio hiyo, na Diamond Platnum ni msanii mwenye mafanikio haswa kuliko wote Tanzania, amepata tuzo nyingi kuliko waimbaji wote wa Bongo fleva, na ndio msanii anaeitangaza Tanzania kimataifa kwa sasa.
Tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya simu ya VODACOM linatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 25/12/2014 siku ya X-mass katika ukumbi wa Dar Live uliopo mbagala jijini Dar. siku hiyo wasanii wote hawa wataonyesha hadharani tuzo zao walizopata katika safari yao kimuziki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni