TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 30 Desemba 2014

SAIDI MITUTU AJIUNGA NA GUSAGUSA MIN BENDI, ASEMA KILICHO MBELE YAKE NI KAZI TU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

               Mpiga gitaa la besi ambae amewahi kufanya kazi katika bendi mbalimbali zikiwemo Dar Modern, Coast Modern Taarab, Aden Modern Taarab na nyinginezo nyinyi "Saidi Mitutu" amejiunga rasmi na bendi ya Gusagusa min bend.

         Akizungumza na mtandao huu Mitutu alisema kwa ridhaa yangu nimeamua kujiunga na bendi hii ili kujiendeleza zaidi na taaluma yangu, jambo lingine ujio wa Meneja Kais Mussa Kais katika bendi hii umenishawishi kwa asilimia kubwa zaidi mimi kufanya maamuzi ya kuja huku, Kais ni kiongozi mwenye historia nzuri hususani katika kila bendi aliyoiongoza imekuwa ikifanya vizuri sana

SAIDI MITUTU.
           Kwa upande wa meneja Kais alisema kwamba hizo ni rasharasha tu mvua kamili inakuja, nimepanga kukisuka upya kikosi changu na tayari nimeshafanya mazungumzo na viongozi wangu nikiwa na maana wakurugenzi wangu Foni Chupa na Hassan Farouk wao kwa pamoja wamenipa uhuru wa kuchagua msanii yeyote ninaeona anafaa kuwa na sisi basi niwajulishe na mara moja atajumuishwa kundini.

GUSAGUSA MIN BENDI KATIKA POZI.
        Wasanii wa zamani wa bendi hii wataendelea kuwepo ingawa kuna taratibu za kuongeza waimbaji na wapiga vyombo pia, Nataka kuifanya gusagusa kuwa ni bendi tishio zaidi na zaidi alimalizia kusema meneja Kais.

                                           "WAKATI HUO HUO"

            Bendi yako ya Gusagusa min bendi siku ya leo katika kuukaribisha mwaka 2015 wanatarajia kufanya show ya nguvu katika ukumbi wa Lango la Jiji uliopo magomeni mikumi jijini Dar wakishirikiana na Aljazira, Raha Original, Sabaha Muchacho pamoja na Bi Mwanahawa Ally. na siku ya tarehe 2/1/2015 Gusagusa min bendi itakuwa Kilwa kivinje katika ukumbi wa kivulini au almaarufu jumba la dhahabu katika kuwapa burudani wakazi wa huko.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni