TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 5 Januari 2015

GUSAGUSA MIN BENDI NDANI YA SAFARI CARNIVAL KILA JUMAPILI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Wataalam wa "Old is Gold" Gusagusa min bendi wamesikia kilio cha muda mrefu toka kwa wakazi wa kawe na kuanzisha program ya burudani kwa wapenzi wa bendi hiyo waishio huko na vitongoji vyake, kwa sasa bendi hii itakuwa ikipatikana katika kiwanja bora na cha wastaarabu cha "Safari Carnival" kila siku ya Jumapili kuanzia saa 2 usiku.

        Akizungumza na mtandao huu Meneja wa bendi hiyo Kais Mussa Kais amesema kwamba bendi ya Gusagusa min bendi imebadilika kwa sasa na ni ya kimataifa zaidi, huko tuendako sasa Safari Carnival ni sehemu maalum na hata maudhui ya sehemu hiyo ni ya kisasa mno. kwa kushirikiana na wakurugenzi wangu Foni Chupa na Hassan Farouk tunawaahidi kuwapa burudani nzuri na ambayo walikuwa wameikosa kwa kipindi kirefu ndani ya maeneo hayo.

         Waimbaji wetu wamejipanga vyema katika kuhakikisha taarab asilia inapatikana na watu wana-enjoy!, tunawaomba mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kwani hii ni program endelevu, jumapili hii ijayo na kila jumapili Gusagusa min bendi tutapatikana ndani ya Safari Carnival, njoo uwaone wakongwe Bi Mwanahawa Ally, Bi Afua Suleiman na hata Sabaha Salum Muchacho pia wakati mwingine huwa anakuja kama msanii mwalikwa.

       Gusagusa min bendi ni bendi ya taarab ambayo yenyewe inapiga ile taarab asilia haswa! ijapokuwa mara chache hupiga hata za kisasa kidogo, bendi hii program yake ni kila ijumaa huwa inapatikana pale Max Bar ilala, vile vile kila Jumamosi huwa inapatikana kiwanja cha nyumbani cha Lango la Jiji magomeni mikumi, na jumapili ndio itakuwa ikipatikana ndani ya Safari Carnival
njoo uwaone na uburudike.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni