TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 5 Januari 2015

MAJA'S MODERN TAARAB KUINGIA KAMBINI JUMATANO IJAYO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Baada ya kutoka katika safari ya kisiwani Mafia, bendi inayokuja kwa kasi kwa burudani za nguvu ya Maja's Modern Taarab inatarajia kuingia kambini jumatano tayari kwa kuandaa nyimbo tatu mpya kabisa ili kwenda sambamba na ushindani wa kibiashara ya muziki wa taarab uliopo kwa sasa hapa nchini.

        Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Hamisi Majaliwa alisema kwanza kabisa napenda niwashukuru wakazi wa kisiwani mafia kwa mapokezi yao mazuri kwetu na nimefurahishwa sana na jinsi walivyojitokeza kwa wingi katika maonyesho yetu mawili ambayo tuliyafanya katika kisiwa hicho.

WAIMBAJI WA MAJA'S MODERN TAARAB WAKIWA STEJINI.
       Vile vile napenda niwajulishe wapenzi na wadau wote wa Maja's Modern Taraab kwamba Jumatano ijayo panapo majaaliwa yake muumba tutaingia kambini na vijana wangu kutengeneza nyimbo tatu mpya ambazo mpaka sasa sijateua ni nani na nani ambao nitawapa nyimbo hizo kuimba, nipo katika mipango ya kuongeza waimbaji wengine wapya na kwa sasa tupo katika mazungumzo na hao waimbaji, mungu akipenda hiyo jumatano wanaweza na wao kuanza mazoezi na wenzao alimaliza kwa kusema mkurugenzi wa Maja's Hamisi Majaliwa.

     Ikumbukwe Maja's Modern Taarab imezaliwa kutoka king's modern taarab baada ya viongozi wake kutofautiana, ila king's mpaka sasa haijajulikana ni lini wataanza mazoezi au show moja kwa moja watafanyia wapi!, ila nawaahidi wasomaji wangu kwamba nitafuatilia maendeleo ya king's mbona wapo kimya mnooo!!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni