TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 1 Januari 2015

HERI YA MWAKA MPYA 2015 WASOMAJI WOTE WA ubuyuwataarabutz.blogspot.com JE NINI MAONI YENU KWA MWAKA HUU?.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Mtandao bora na makini kabisa wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Unaoongozwa na Kais Mussa Kais kwa pamoja na dawati zima la habari, unapenda kuwapongeza wasomaji wake kwa kusherehekea vyema mwaka mpya wa 2015 kwa amani na utulivu mkubwa.

          Ni mambo mengi magumu ambayo mmepitia katika mwaka uliopita wa 2014, na wapo ambao wameweza kufanikiwa katika mwaka huo lakini yote kwa yote inabidi tuanze sasa kujipanga kwa safari ya mwaka huu wa 2015 ambao ni matumaini yetu utakuwa ni wa mafanikio zaidi.

        Kwa upande wa mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com tunawaomba wasomaji wetu kuendelea kutuunga mkono kwa kusoma habari zetu na pia kutushauri ni jambo gani la kupunguza na jambo gani la kuongeza ili kuweza kukidhi matakwa ya ninyi wasomaji wetu japo kwa asilimia kadhaa. Tunaamini wazi kwamba sisi bila ninyi si lolote wala si chochote hivyo basi tupo tayari muda na wakati wowote kupokea ushauri toka kwenu. Mwisho kabisa tunapenda kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2015 mungu awabariki nyote!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni