TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 27 Agosti 2015

AISHA MASANJA:- SITOSAHAU SIKU NILIPOKAUKIWA SAUTI NIKIWA NAIMBA STEJINI ZANZIBAR STAR'S.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Aisha masanja ni jina lililojizolea umaarufu mkubwa katika tasnia hii ya taarab nchini tanzania kwa miaka kadhaa sasa, muimbaji huyu amekuwa kimya kwa muda hali iliyopelekea wadau kutaka kujua yupo wapi kwa sasa.


AISHA MASANJA.

       Dawati la habari la mtandao huu lilimtafuta ili kutaka kujua ni kipi kimemsibu mbona kimya kimezidi sana na wadau wa taarab wamemiss kazi zake nae alikuwa na haya ya kujibu, kwa sasa sina bendi yoyote nipo tu nyumbani ingawa wakati mwingine huwa naisaidia bendi ya coast modern taarab, kuna kipindi fulani nilikuwa katika mazungumzo na bendi ya supershine modern taarab lakini mwisho wa siku hatukufikia muafaka ikabidi niendelee kubaki nyumbani.unajua tokea nimetoa wimbo wa ubaya una mwisho nikiwa na T motto sijarekodi tena ni zaidi ya miaka mitatu. tokea niingie katika tasnia hii ya taarab nimefanikiwa kurekodi nyimbo tatu ambazo ni, Asieumba haumbui-coast modern taarab, Ridhiki shotcut- t motto na huu Ubaya una mwisho ambao pia nimeimbia t motto.


        Nipo katika maandalizi ya kufanyia mazoezi wimbo mpya na nitauimba hapa coast modern taarab nyumbani ila sijajua mpaka sasa mashairi yataitwa vipi naomba wadau na wapenzi wangu waendelee kuvuta subira nakuja kivingine sasa. Jambo ambalo limeendelea kukaa katika kichwa changu ni lile tukio la kukaukiwa sauti nikiwa stejini naimba pale zanzibar star's modern taarab, nashangaa ni nini ilikuwa maana mpaka sasa jibu sipati ingawa ni miaka mingi imepita, sitaki kuamini kuwa ilikuwa ni ushirikina kwakweli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni