TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 27 Agosti 2015

MAINA THADEI:- NI UZUSHI TU WA WALIMWENGU...MIMI SINA MIMBA NIPO SHWARI!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Kwa sasa unapolitamka jina la maina thadei katika tasnia hii ya taarab nchini basi kila mmoja anajua wazi kuwa huyo ni muimbaji machachari toka katika bendi ya exellent modern taarab iliyo na maskani yake jijini dar.


MAINA THADEI-MUIMBAJI WA EXELLENT MODERN TAARAB.

         Siku za karibuni kumekuwa na habari zilizotapakaa miongoni mwa wadau wa tasnia hii ikimuhusisha muimbaji huyu kuwa tayari ndoa yake na muimbaji mwenzie toka bendi hiyo mwinyi mkuu imejibu na bibie anakula ndimu hatari!, kama kawaida ya mtandao huu ulipiga hodi mpaka mikocheni MRC yalipo makazi ya ma-superstar hawa na kubahatika kufanya mahojiano ya ana kwa ana na maina mwenyewe juu ya habari hii ni kweli? na ikiwezekana tuandae zawadi kwa ajili ya mtoto! nae alikuwa na haya yakuzungumza.


      Ndugu mwandishi kwanza naomba nikanushe habari hizi kuwa si kweli, mimi nipo poa sina mimba kabisa, na uvumi huu umeanza baada ya mimi kuugua maralia kali sana iliyopelekea nikawa sitokei mazoezini mpaka katika show!. nawaambia mashabiki zangu kuwa nipo shwari sina ujauzito na waje katika uzinduzi wetu hapo tarehe 4/9/2015 katika ukumbi wa mikocheni resort nitakamua ile mbaya. unajua mimi napenda sana mtoto ila bado mwenyezimungu hajanijalia ikitokea siku nimepata mimba basi nitapiga na picha kabisa kuwajuza mashabiki kuwa sasa ndoa imejibu wasiwe na wasiwasi juu ya hilo nawapenda sana!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni