TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 27 Agosti 2015

HAMUYAWEZI KONDO MAMAA "KALIENI VITI SIO UMBEA" AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

               Muimbaji wa bendi ya wakaliwao modern taradance Hamuyawezi kondo ambae ndie muimbaji wa wimbo wa kalieni viti sio umbea amejifungua salama mtoto wa kiume alfajiri ya kuamkia jana.


HAMUYAWEZI KONDO.

        Akizungumza na mtandao huu mume wa muimbaji huyo mr ochu kilimba alisema kuwa alimpeleka mkewe hospitali muda wa saa tisa alfajiri na ilipofika saa kumi alfajiri mkewe alijifungua mtoto wa kiume salama usalimini, namshukuru mungu kwa kumuwezesha mke wangu kujifungua bila matatizo, mtoto mpaka sasa bado sijampa jina nasubiria wajomba zake ndio watatoa jina...unajua tena mambo ya mila lazima yaenziwe.


        Sisi mtandao wa ubuyu wa taarab tunapenda kuchukuwa nafasi hii kumpongeza Hamuyawezi kondo kwa kufanikiwa kupata mtoto wa kiume na mungu ampe afya njema yeye pamoja na mtoto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni