Mtangazaji wa kipindi cha taarab cha "kwa raha zangu" kinachorushwa na redio pwani fm mombasa kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa sita hadi saa nane mchana Bishara aden amelalamika kutapeliwa pesa zake na muimbaji wa Dar modern Hassan vocha.
Akizungumza kwa uchungu mkubwa bishara alisema kuwa alikuwa akiwasiliana sana na hassan vocha kwa njia ya simu na kufanya nae interview kutokana na kazi zake ambazo yeye kama mtangazaji amekuwa akizicheza redioni, kuna siku hassan vocha akanitumia voice katika whatsap yangu akilia kuwa mama yake anaumwa huko kigoma na hana pesa ya kumtumia ili apelekwe hospitali, akaniomba mimi nimkopeshe pesa, mimi sikuwa na pesa kipindi hicho ila nilimuahidi nitakopa kwa mtu ili nimtumie amalize shida zake ila baadae zirudi kwani na mimi pia nimekopa.
Kweli anasema alimtumia na hassan vocha kukiri kwa njia hiyo hiyo ya voice kwamba amezipata pesa hizo, baada ya kupita siku mbili hassan akatuma voice ingine akisema kuwa yule mama yake amekufa huko kigoma na yeye hana pesa ya kumfikisha kigoma kwa ajili ya mazishi hivyo kwa mara ingine aliniomba tena nimtumie pesa ili awahi kuzika lakini pindi atakapokuwa amerudi atanirudishia, nikaona sawa haina shida kwakuwa sikuwa na pesa zote za kumpa kipindi kile nikamwambia nitakutumia nauli ya kukufikisha kigoma tu alafu wakati unataka kurudi uniambie nitakutumia pesa ingine ili urudi...akasema sawa, lakini nikaanza kupatwa na wasiwasi juu ya taarifa zake, kama ujuavyo huko tanzania nina marafiki kibao nikaanza kufanya uchunguzi wangu na kugundua kuwa hassan alikuwa akinitapeli tu hajasafiri na yupo hapo hapo dar, kwakweli iliniuma sana! kwanini aniongopee? ukimuangalia katika instagram kila siku yupo active na anaposti video zake mpya kama kawaida, nilipojaribu kukumbushia pesa zangu amekuwa akini rusharusha kila wakati, sijalipwa mpaka sasa na hakuna mategemeo ya kulipwa mpaka muda huu!.
![]() |
HASSAN VOCHA. |
Mtandao huu ulimtafuta hassan vocha na kumuuliza juu ya tuhuma hizi nae alikuwa na haya ya kusema, kwanza ni kweli bishara alinipa pesa hizo baada ya kufikwa na matatizo ya kufiwa na mama yangu na ni kweli nilienda kigoma kuzika, ila kilichotokea bishara amekuwa akiwasiliana na mtu huku tanzania ambae mimi simfahamu na amekuwa akimpa taarifa zisizo za kweli juu yangu, mimi siwezi kumdhurumu pesa zake na nitamrudishia ijapokuwa muda niliomuahidi kumlipa pesa zake umepita. mimi ni mtoto wa kiislam na nina imani haswa ya dini siwezi kumdhurumu!, namuomba awe anajibu sms zangu za whatsap ili tuweze kuyamaliza haya matatizo alimaliza kwa kusema hassan vocha!.
![]() |
BISHARA ADEN AKIWA STUDIO. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni