TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 27 Novemba 2015

KWA MARA YA KWANZA WAKALIWAO MODERN TARADANCE, NDANI YA HIZZA HALL MAJOE TAREHE 6/12/2015

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Bendi bora na inayofanya vizuri kwa sasa kuliko bendi yoyote hapa nchini, wakaliwao modern taradance, kwa mara ya kwanza inatarajia kufanya show ya nguvu katika ukumbi wa hizza hall uliopo maeneo ya majoe bwela nje kidogo ya jiji la dar.

           Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Thabit abdul alisema kuwa vijana wake wamejipanga vyema katika kuhakikisha wanakonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wao waliopo maeneo hayo, siku hiyo tutapiga nyimbo zile za zamani kama kalieni viti sio umbea mpaka hizi mpya ambazo zinatamba kwa sasa katika vituo mbalimbali vya redio nchini. hii show si ya kukosa kwani pamoja na sisi wakaliwao lakini pia tutasindikizwa na msagasumu pamoja na dogo jack simela alimaliza kwa kusema.

        Show itaanza saa kumi kamili jioni na kumalizika saa sita usiku, kiingilio itakuwa wakubwa 5000/= na watoto ni shilingi 2000/=, hili ni bonanza la nguvu kwa wakazi wa majoe na vitongoji vyake, fika uwashuhudie wakaliwao modern taradance kwa mara ya kwanza ndani ya viwanja vya hizza hall majoe bwela.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni