Watangazaji wa kipindi cha taarab kiitwacho "tashititi zetu" ndani ya uhuru fm Mc jojoo na Nuru issa wa suleiman wakishirikiana na wadhamini uhuru fm wenyewe, mc jojoo entertainment, ubuyuwataarabutz.blogspot.com, nasreen cosmetics, aunt latifah catering, ranessa travel tour na sinai clinic wameandaa tamasha liitwalo "kitchen party dawa" unyago unyagoni ambalo litafanyika katika ukumbi wa dar west tabata jijini dar siku ya ijumaa tarehe 11/12/2015.
![]() |
MTANGAZAJI WA UHURU FM "TASHITITI ZETU" MC JOJOO TANZANIA. |
Wakizungumza na mtandao huu makini waandaaji hao walisema kuwa nia na madhumuni haswa ya tamasha hilo ni kukumbushana au kupeana somo juu ya mambo ya ndani, pia kutakuwa na mada mbalimbali za kimaisha, kwa wanawake na wanaume ambao wana matarajio ya kuingia ndoani na hata wale ambao wapo na wapenzi au wachumba, pia burudani itahusika zaidi pale kati kwa bendi kadhaa kutumbuiza ambazo ni Excellent modern taarab, kibao kata, Abdul misambano, jokha kassim, wakali wa masauti, isha mashauzi pamoja na watoto ambao wanaishi na virusi vya ukimwi nao watakuwepo.
![]() |
MTANGAZAJI WA UHURU FM "TASHITITI ZETU" NURU ISSA WA SULEIMAN. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni