NA KAIS MUSSA KAIS
Msanii Mkongwe katika
tasnia ya muziki wa Taarab asilia mwenye asili ya Mombasa ambaye pia
alikuwa mwenye uwezo wa kutunga mashairi, kuimba huku akipigia
kinanda Mohammed Khamis Juma Bhalo maarufu kama Profesa Juma Bhalo, ambapo alifariki mnamo tarehe
5/4/2014 na kuzikwa Jumapili tarehe 6/4/2014.
ubuyuwataarabutz,blogspot.com ilizungumza na mtoto wa
mwisho yaani Kitinda Mimba wa marehemu Profesa Juma Bhalo
anayefahamikia kwa jna la Ahmed Juma kwa njia ya simu kutoka Mombasa, ambaye alisema alifariki baada
ya kuugua kwa muda mfupi, na alizikwa kwenye makaburi ya Kikoani.
Akizungumzia juu ya mtoto
ambaye ameweza kufata nyayo za baba yake Profesa Juma Bhalo alisema
ilikuwa vigumu sana kwa baba yake kukubali mwanaye kufata nyayo zake
japokuwa baadaye alimkubalia miongoni mwa wanawe hao kufata nyayo
hizo, fahamu pia asili hasa ya marehemu Juma
Bhalo.
-Alizaliwa
mwaka 1940 mtaani shela eneo la malindi katika Pwani ya Kenya
MAREHEMU PROFESA JUMA BHALO ENZI YA UHAI WAKE |
Na
amefariki akiwa na umri wa miaka 74 , na kutokana na hali ya maisha
ya wazazi wake hakuweza kuendelea na masomo hivyo aliishia darasa la
4 na kuendeleza masomo ya madrasa, lakini pia hakuweza kumaliza
masomo hayo kutokana na ugumu wa hali ya maisha pia.
Ameacha
wajane wawili, watoto 14 japokuwa alibahatika kupata watoto 17 lakini
watatu wametangulia mbele ya haki.
Alianza
kuimba Mwaka1957, na 1mwaka 1966 alianzisha kikundi chake
kilichoitwa Bhalo and Party huku akisaidiana na Malenga wa Mvita.
Alikuwa na uwezo wa kukariri nyimbo za Kihindi na kuziimba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni