NA KAIS MUSSA KAIS.
Laiti kama ungepata bahati ya kuwaona vijana wa wakaliwao wakiwa mazoezini kujifua kwa ajili ya tamasha kubwa la taarab "mitikisiko ya pwani" linalo tarajiwa kufanyika pale katika ukumbi wa dar live mbagala jijini dar ungeridhika na nafsi yako.
Show maalum ya wacheza viduku sambamba na step's bab-kubwa ambazo walikuwa wakizifanyia mazoezi inatosha kukuthibitishia wazi kuwa kwa sasa wakaliwao modern taradance ndio gumzo la jiji kutokana na ubora wao wanapokuwa stejini, vijana hao ambao wapo sita wakiume watano na wakike mmoja wanapokuwa wanacheza utatamani japo kuwasogelea ili kuthibitisha vile ni viuno vyao ama pangaboi,
Kwa upande wa waimbaji wakaliwao kwa sasa wana ubora mkubwa sana kulingana na wasichana wengine walioongezwa kama Aisha othman vuvuzela, salha wa hammer Q, kibibi yahya, Asia mjusi sambamba na Aisha mtamu kabisa muimbaji gumzo kwa sasa town!.
Akizungumza na mtandao huu thabit abdul mkurugenzi wa bendi hiyo alisema kuwa kamwe hawatorudia makosa kama ya mwaka jana ambapo iliwaladhimu kutopanda stejini kwa kosa la wasanii kuchelewa ukumbini, nitahakikisha hali ile haijitokez
i tena alimaliza kwa kusema, tamasha la mitikisiko ya pwani linatarajiwa kufanyika leo baadae katika ukumbi wa dar live kwa kiingilio cha elfu kumi tu!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni