TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 7 Juni 2015

YUSUPH TEGO:- COAST MODERN TAARAB IMENIFANYA NITAMBULIKE ZAIDI KISANAA!.


NA KAIS MUSSA KAIS.

           Wapenzi wasomaji wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com habari za mwisho wa wiki, leo tumekutana tena katika hiki kipengele chetu cha mjue msanii wako kama ilivyo ada yetu. Na leo tunae Yusuph Tego ukipenda muite "mzungu wa london" mpiga kinanda wa coast modern taarab, twende nae sambamba katika kumfahamu ametokea wapi mpaka kufikia alipo.


        Jina langu kamili ni Yusuph Tego hilo la mzungu wa london nimepewa na mashabiki wangu tu kulingana na kazi nzuri ninayoifanya, nimeanza muziki huu wa taarab rasmi kabisa mwaka 2000 katika bendi ya Coast modern taarab, hii ni bendi ya nyumbani kwetu kabisa na kipindi cha nyuma ilikuwa inaongozwa na mzee tego mwenyewe. Hapa naweza kusema ni sehemu nilipojifunzia muziki huu kwa mara ya kwanza kupitia kwa kaka yangu Omary Tego mpaka kufikia hapa nilipo.


    Katika bendi ya coast modern taarab nimekaa kwa kipindi kirefu nikijifunza muziki mpaka pale nilipoonekana sasa nimewiva ndipo nilipokabidhiwa wimbo wa gubu la mawifi ulioimbwa na dada yangu "Maua Tego" nikarekodi mimi kinanda kwa mara ya kwanza, namshukuru mungu wimbo ule ulipokelewa vizuri sana na wapenzi wa taarab na wadau, ikawa ndio chanzo cha safari yangu ya kimuziki.

YUSUPH TEGO "MZUNGU WA LONDON".

  Mwaka 2013 nilihamia katika bendi ya five star's modern taarab ili kwenda kuongeza kipaji changu zaidi, na pale nilikutana na wapiga vinanda wazoefu kama Thabit Abdul, Ally J na Juma Mkima tukafanikiwa kutengeneza albam moja ambayo ilifanya vizuri sana sana chini yake mkurugenzi "Shark's the Don", mwaka huo huo katikati nikapata safari ya kwenda Dubai kupiga muziki katika mahoteli mbalimbali yaliyopo huko, nikaenda zangu.


    Mwaka 2014 nilirudi Tanzania na kujiunga na vijana wa Yamoto bendi ambayo ipo chini ya mkubwa fellah ambayo ipo maeneo ya temeke, pale nilikaa kwa muda mchache na pia nilifanikiwa kurekodi nao nyimbo kadhaa ambazo bado hazijaanza kutambulishwa maredioni. kwa sasa nimeamua kuachana nao yamoto bendi na nimeamua kurudi nyumbani yaani Coast modern taarab na nipo na brother angu Omary Tego na sister Maua tego. tunaanda nyimbo zetu mpya ambazo nadhani baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa ramadhan tutaanza kuzitambulisha rasmi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni