TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 13 Desemba 2015

SHANGWE ZA X-MASS NA WAKALIWAO MODERN TARADANCE RATIBA KAMILI NI HII.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Bendi yako uipendayo ya wakaliwao modern taradance baada ya kufanya vizuri katika tamasha la mitikisiko ya pwani hapo jana ndani ya ukumbi wa dar live mbagala jijini dar, leo wametoa ratiba yao kamili katika kusherehekea sikukuu ya x-mass.

            Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema kwamba siku ya mkesha wa sikukuu hiyo yaani tarehe 24/12/2015 alhamisi wakaliwao watashusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa bagamoyo view  "macho kodo" uliopo bagamoyo mkoani pwani, siku ya tarehe 25/12/2015 ijumaa yaani siku yenyewe ya sikukuu ya x-mass bendi hiyo itawasha moto wa burudani katika ukumbi wa "fanya fasta" uliopo boko nje kidogo ya jiji la dar, katika siku zote hizo wakaliwao watatambulisha nyimbo zao mpya zikiwemo ukinuna uwe na sababu ulioimbwa na aisha othman "vuvuzela", old fashion ulioimbwa na kibibi yahya, najuta kupenda ulioimbwa na muimbaji mpya wa bendi hiyo aisha mtamu kabisa sambamba na nyimbo zingine mpya mbili ambazo zimeimbwa na hashim said na asia mjusi zitatambulishwa pia alisema.

               Alimalizia kwa kusema kuwa wapenzi na wadau wa wakaliwao modern taradance nawaomba wajitokeze kwa wingi kwani pamoja na wakaliwao lakini kutakuwa na wasanii waalikwa ambao ni msagasumu na dogo jack simela mfalme wa miondoko ya mnanda tanzania kwa sasa. kiingilio katika show zote hizo itakuwa ni shilingi elfu tano tu 5000/= nyote mnakaribishwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni