TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 13 Desemba 2015

ISOME HII:- MWAMVITA SHAIBU AJIUNGA RASMI NA OGOPA KOPA CLASSIC BENDI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                   Mwamvita shaibu muimbaji wa zamani wa zanzibar stars, five star's na dar modern taarab amejiunga rasmi katika bendi ya ogopa kopa na jana alikuwepo katika jukwaa la ogopa kopa akiwajibika kama kawaida.


MWAMVITA SHAIBU AKIWA STEJI.

             Mwandishi wa habari hzi alipata taarifa hizi mapema hata kabla wasanii wa ogopa kopa hawajaingia ukumbini kwahiyo alichofanya ni kumuwinda mwamvita shaibu maeneo ya mlangoni ili akifika afanye nae mahojiano kabla hajaingia ukumbini ambapo kusingekuwa na usikivu. Ilipofika muda wa saa mbili kasoro ogopa kopa waliingia na ndipo alipomvuta pembeni na kumrekodi maongezi yake, kwa upande wake mwamvita shaibu alikili kuwa kwa sasa yeye ni msanii wa ogopa kopa ila hajasaini mkataba zaidi ya kuingia makubaliano tu na uongozi wa bendi hiyo na mpaka sasa yupo mazoezini kufanya mazoezi ya wimbo wa "ushoga ndui" ambao anatarajia kuurekodi siku chache zijazo.


          Nae mkurugenzi wa bendi hiyo khadija omary kopa alisema kwamba ni kweli nimeamua kumuongeza mwamvita shaibu sababu ana uwezo mkubwa na sio vibaya kama atakuwa ni mmoja wa waimbaji wangu. kwa sasa nipo nae na hivi karibuni ataingia studio kurekodi wimbo wake wa kwanza akiwa na ogopa kopa alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni