TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 13 Desemba 2015

HII NI TATHMINI YA TAMASHA LA MITIKISIKO YA PWANI 2015 LILILOFANYIKA JANA JUMAMOSI TAREHE 12/12/.

NA KAIS MUSSA KAIS.
      0657-036328.
MAINA THADEI WA EXCELLENT AKICHEZA NA WACHEZA SHOW WAKE.

                  Ilikuwa ni kama siku ambayo timu kubwa hapa nchini za simba na yanga zinapokutana katika ligi kuu ya mpira wa miguu, umati uliojitokeza kushuhudia tamasha hilo ni mkubwa sana ambao nahisi ulipita hata makisio ya waandaaji yaani times redio ya jijini dar...hongera sana kamati nzima ya maandalizi.
PICHA TOFAUTI WAKALIWAO WAKIWA JUKWAANI.
                  Tamasha lilianza saa mbili na dakika 45 kwa utangulizi wa vijana wa bongo fleva kupanda steji na kuimba wimbo maalum wa kusifia tamasha hilo, baadae ndipo naweza kusema tamasha lilifunguliwa rasmi kwa vijana wa kibao kata chini ya mtaalam dogo kivurande junior walipopanda stejini na kufanya yao kwa takribani dakika 45, waliwachengua watu kwa nyimbo zao zenye mafumbo tata na zinazochezeka na kuleta radha zaidi, ndipo walipofuata excellent modern taarab chini yake mwinyimkuu na mkewe maina thadei kupanda stejini na kufanya yao kwa kuimba nyimbo tatu mfululizo pasipo kushuka stejini, watu waliwashingilia sana kwa umahiri haswa wa maina thadei kuzungusha nyonga kisawasawa jambo lililofanya wapenzi kulipuka kwa shangwe kubwa, ikumbukwe vijana wa excellent modern taarab hili ni onyesho lao la kwanza kubwa zaidi kushiriki lakini walionekana kujiamini zaidi na kufanya vizuri sana, hongereni mwinyimkuu na maina thadei kwa kazi nzuri sana.

MFALME MZEE YUSUPH AKIIMBA STEJINI.

          Waliposhuka stejini alisikika Mc pilipili akiwauliza mashabiki je ni bendi ipi wanata ipande stejini kwa muda huo kati ya ogopa kopa na wakaliwao?, mashabiki walilipuka kwa shangwe na kutaka wakaliwao ndio wapande lakini badala yake Mc pilipili aliwapandisha njenje chini ya nyota waziri na kuwadhihirishia mashabiki kuwa wao ni wataalam wa burudani hapa nchini, walitumbuiza kwa muda wa saa moja nzima na kufanya mashabiki kuviacha viti vyao kwa muda ili kucheza nao kwa pamoja.baada ya kushuka wana njenje wakapanda ogopa kopa classic na aliefungua kwa waimbaji wa ogopa kopa ni malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa ambae aliimba wimbo wa "mamaa mukubwa" na kushangiliwa kwa nguvu mno, baadae aliimba black kopa ambae aliingia kama mtoto wa mfalme haswa huku akitandikiwa zulia na kuimba chini ya ulinzi wa vijana wawili waliovaa kama walinzi wa jumba la mfalme, alimalizia kuimba  shadya shombeshombe ndipo muda wao ukawa umeisha, lakini yalisika malalamiko toka kwa mashabiki wakilaumu ni kwanini young hassan ally na khanifa maulid "jike la chui" hawakuimba huku wakiwa wapo humo katika onyesho?.

NYOTA WAZIRI WA NJENJE AKISEREBUKA SAMBAMBA NA SHABIKI WAKE.
                          Wakaliwao modern taradance walipanda stejini baada ya kushuka ogopa kopa, nao walianza kwa show ya wacheza viduku wao kwa takribani dakika tano ndipo baadae alianza kuimba Aisha mtamu kabisa wimbo wa "najuta kupenda", mashabiki walimshangilia sana kwa umahiri wake wa kuimba na kucheza ukizingatia ni msanii mdogo kuliko wote ndani ya wakaliwao, baadae aliimba mwalimu nassoro wimbo wa sweet baby kwa dakika ishirini na kushangiliwa pia, mwisho wakaliwao walimpandisha Aisha othman vuvuzela na wimbo wake mpya usemao "ukinuna uwe na sababu", wapenzi walishindwa kuzuia hisia zao nakujikuta wakiimba sambamba na muimbaji huyo ingawa ni wimbo mpya!, naweza kusema wakaliwao walifanya vizuri sana zaidi ya sana...hongera sana thabit abdul kwa ulichokifanya na vijana wako.

MA-MC WA SHUGHULI HIYO DIDA SHAIBU NA MC PILIPILI WAKIWA KWENYE POZI.

                 Baadae alipanda msagasumu mfalme wa uswazi, kabali yao! ambae aliwapagawisha mashabiki kwa nyimbo zake tamu na nzuri zinazotamba sana kwa sasa katika media mbalimbali hapa nchini na hata afrika mashariki kwa ujumla, aliposhuka msaga sumu alipanda Dogo S. kide na nyimbo zake zenye mtindo wa kisingeli, alishangiliwa sana na kuwarusha mchakamchaka masela wote waliojitokeza katika tamasha hilo.

MALIKIA KHADIJA OMARY KOPA AKIWA NA HEMEDY OMARY MC WA OGOPA KOPA.

                                Baadae walipanda jahazi modern taarab chini ya mfalme mzee yusuph na kuamsha shangwe na nderemo nyingi toka kwa mashabiki na wapenzi wa bendi hiyo ambao walionekana kusubiri kwa hamu zamu ya jahazi ifike waburudike kwa raha zao, nao jahazi walikamua nyimbo tatu safi kabisa na kuwaacha mashabiki wao wakiwa ni wenye furaha kwa burudani hiyo, mtandao huu unapenda kumpongeza mzee yusuph kwa kilewalichofanya jana maana kila aliekuja aliondoka akiwa ameridhika kabisa. waliohitimisha tamasha hilo muda wa saa tisa usiku ni wana kibao kata chini ya kivurandejunior ambao naweza kusema walirudi kwa mara ya pili mfululizo.

WACHEZA SHOW WA KIBAO KATA NAO WALIWADATISHA MASHABIKI.

                                               "MAPUNGUFU YALIYOJITOKEZA".

MSAGASUMU KABALI YAO AKIFANYA YAKE STEJINI.
                           Pamoja na mazuri yote yaliyofanywa na kamati iliyoandaliwa na redio times fm lakini kulikuwa na mapungufu machache yaliyojitokeza ambayo ni kukatika mara kwa mara kwa umeme katika ukumbi huo, umeme ulikatika zaidi ya mara tatu huku bendi kadhaa zikiwa stejini zikipafomu, lingine ni mice ya wireless iliyokuwaikitumika kuimbia ilikuwa ikikatakata kila wakati jambo lililopelekea baadhi ya waimbaji kutosikika walichokuwa wakiimba, vile vile kulikuwa na uhaba mkubwa wa viti vya kukalia jambo lililopelekea baadhi ya mashabiki japo walilipa kiingilio cha elfu kumi lakini walijikuta wakikosa pa kukaa!. lakini yote kwa yote uongozi wa mtandao huu unapenda kuwa pongeza times fm kwakufanikiwa kwa asilimia kubwa juu ya tamasha lile...tukutane tena mwakani panapo majaaliwa yake mola inshallah!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni