TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 17 Desemba 2015

HAMUYAWEZI KONDO NA FARIDA KINDAMBA WAJIUNGA NA MAJA'S MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Waimbaji wawili hamuyawezi kondo na farida kindamba wamejiunga na bendi ya maja's modern taarab wakitokea wakaliwao modern taradance.


HAMUYAWEZI KONDO-MUIMBAJI MPYA WA MAJA'S MODERN TAARAB.

         Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu bora wa ubuyu wa taarabu, mkururugenzi wa maja's modern taarab Hamisi majaliwa alisema ni kweli wasanii hao ni miongoni mwa wasanii wapya ambao wanaunda bendi hiyo,nimefanya usajili bab-kubwa na nawaomba wadau wajiandae kupokea vibao vipya toka kwetu, alipoulizwa wasanii hao wamesaini mkataba wa miaka mingapi?, yeye alisema hiyo ni siri ya uongozi na hayupo tayari kuanika hadharani ila kikubwa wafahamishe wapenzi kuwa wasanii hao kwa sasa wapo maja's.


          Mtandao huu ulimuendea hewani mkurugenzi wa wakaliwao thabit abdul ili kutaka kujua kuwa je na yeye ana taarifa za wasanii hao kujiunga na maja's modern taarab? alijibu kuwa yeye anasikia tu juu juu na wala hana habari kamili na kama ni kweli basi namuomba majaliwa brother angu aje tukae tuzungumze kiurafiki tu kwani mtu kama hamuyawezi kondo ana mkataba wa miaka miwili na wakaliwao na ushahidi upo wazi kabisa kwenye makaratasi, ila upande mwingine simzuii msanii yeyote kuhama bendi hii kilichopo utaratibu unatakiwa ufuatwe tu kwa wale wenye mkataba.

FARIDA KINDAMBA-MUIMBAJI MPYA WA MAJA'S MODERN TAARAB.


         Mtandao huu ulipopata majibu hayo ulipiga tena simu kwa majaliwa na kumueleza kuwa kwa mujibu wa maelezo ya mkurugenzi wa wakaliwao thabit abdul ni kwamba hamuyawezi kondo ana mkataba wa miaka miwili je wakati anatia saini hapo maja's aliwahi kukuambia hilo?. Yeye alijibu kuwa hakuambiwa jambo hilo na hata kama atakuwa na mkataba na wakaliwao lakini yeye hayupo tayari kumuachia hamuyawezi kwa vyovyote vile, huyo thabit alipowachukua waimbaji wangu salha na kibibi hata mimi niliumia kwahiyo kwa sasa inabidi atulie tu alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni