TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 18 Desemba 2015

WAKALIWAO MODERN TARADANCE NDANI YA KISARAWE NA CHANIKA MKESHA WA MWAKA MPYA!.

NA KASI MUSSA KAIS.


           Bendi yako bora ya wakaliwao modern taradance inaendelea kusambaza burudani zake zenye ubora na safari hii ni kisarawe na chanika katika kusherehekea mwaka mpya wa 2016.


          Uhondo utaanzia pale katika ukumbi wa tausi pub kisarawe katika mkesha wa mwaka mpya yaani siku ya alhamisi tarehe 31/12/2015 na siku inayofuata yaani ijumaa tarehe 1/1/2016 wakaliwao modern taradance itashusha burudani ya nguvu ndani ya ukumbi wa butiama hall uliopo chanika, katika show zote mbili bendi hiyo itashusha kikosi kizima kilichosheheni waimbaji bora na wenye sauti tamu wakiwemo aisha othman "vuvuzela", aisha mtamu kabisa, kibibi yahya, salha wa hammer Q, wamoja salum, nasra shabban, asia mjusi, mwalimu nassoro na hashim saidi "igwee".


      Katika show zote hizo mbili wakaliwao modern taradance itasindikizwa na msagasumu pamoja na dogo jack simela mtaalam wa mnanda tanzania, kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu tano tu nyote mnakaribishwa bila kukosa.

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni