TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 27 Juni 2015

MAJA'S MODERN TAARAB:- HATUTISHIKI NA MAJINA YA BENDI...SISI HAPA KAZI TU MAJUNGU TUNAWAACHIA WAO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Wadau na wapenzi wa taarab walikuwa wanajiuliza kulikoni tena mbona bendi hii ya Maja's modern taarab wapo kimya sana?, lakini wiki hii mkurugenzi wa bendi hiyo aliibuka ofisini kwetu na kuleta nyimbo zake za taarab Audio na video ambazo nimekuwa nikiziweka humu mtandaoni, amesema kwamba bado wapo na wana mambo mengi mazuri wameshayaandaa kwa ajili ya wadau na wapenzi wa bendi hiyo!.


WAIMBAJI WA MAJA'S MODERN TAARAB WAKIWA STEJI.

     Akizungumza kwa kujiamini mkurugenzi huyo Hamisi Majaliwa alisema, baada ya bendi hii kuonekana kama inaanza upya kufuatia ule muunganiko wa iliyokuwa King's modern taarab kuvunjika ilinibidi nikae chini na uongozi wangu mpya wa Maja's modern taarab na kupanga mashambulizi nini tufanye ili kuweza kuwaridhisha wapenzi wa taarab! na tayari tuna nyimbo mpya zipatazo nne huku zingine tayari zikiwa zimeshafanyiwa shooting kama ya Mrisho Rajab B.s.s. na zingine tunatarajia kuzifanyia ndani ya mwezi huu wa ramadhani.


ANAITWA KIBIBI YAHYA, YEYE NI MUIMBAJI NA MATRONI WA BENDI HII YA MAJA'S MODERN TAARAB.

    Aliendelea kwa kusema kwamba wale waimbaji wote ambao walikuwa wakiunda bendi ya King's modern taarab kipindi kile wapo huku kwangu Maja's modern taarab. waimbaji kama vile Mwanahawa Ally "chipolopolo", Kibibi Yahya, Mrisho Rajab B.s.s., Amina Mnyalu na wengineo bado wapo wanaendelea kupiga kazi! kifupi naweza kusema kikosi changu hakijayumba kipo makini kabisa!, mungu akipenda ndani ya sikukuu ya Idd tunaweza kuwa mkoani kufanya show, bado tupo katika mazungumzo na promota flani nisingependa kumtaja jina kwa sasa, ili kuona je tunaweza kuafikiana ama lah! kikubwa ni maslahi ya wasanii wangu tu! kwa yeyote ambae atahitaji lolote toka kwa Maja's modern taarab basi namba yangu mimi mkurugenzi ni hii 0715-451 853 tuwasiliane alimaliza kwa kusema!..


MAJA'S MODERN TAARAB WAKISEREBUKA STEJINI.

    Ikumbukwe kwamba Maja's modern taarab ilizaliwa baada ya iliyokuwa King's modern taarab ya wakati huo kuvunjika baada ya viongozi kutofautiana, unaweza kuona mfano wimbo wa "Hisani nuksani" inatajwa king's lakini humu katika mtandao nimeuandika ni mali ya Maja's modern taarab, haya ni makubaliano ya viongozi hawa wawili yaani Hamisi majaliwa kwa maja's na Kijoka kwa king's ya sasa. inamaanisha kuna vitu wamekubaliana ikiwemo nyimbo hiyo ya Mwanahawa Ally "Chipolopolo" kuwa ya Maja's modern taarab . Mtandao huu wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com unapenda kuwatakia mafanikio bendi ya Maja's modern taarab katika harakati zao za kuja upya na kivingine zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni