Malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa ambae ni mkurugenzi wa ogopa kopa classic bendi amemkana young hassan ally kuwa si director wa bendi kwa sababu director jukumu lake ni kujua maendeleo ya bendi, kama kuna nyimbo mpya ama kuna mazoezi ya umuhimu lakini si kwa hassan ally.
![]() |
MALKIA WA MIPASHO NCHINI-KHADIJA OMARY KOPA. |
Aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi katika tamasha la mitikisiko ya pwani ambalo lilifanyika wiki iliyopita katika ukumbi wa dar live mbagala jijini dar, bendi yangu haina director katika uongozi wa wasanii, hassan ally hajui mazoezi yanaendaje, hajui kuna nyimbo mpya, hajui kama kuna msanii mpya, haudhulii mazoezi sasa huyo utamuita ni director alihoji? sina director katika bendi yangu nasisitiza tena naomba nieleweke!.
YOUNG HASSAN ALLY. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni