TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 18 Desemba 2015

PATA PICHA "12" ZA ONYESHO LA WAKALIWAO MODERN TARADANCE NA MAPACHA WATATU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


           Onyesho lililopewa jina la "usiku wa maswahiba" kati ya wakaliwao modern taradance na mapacha watatu lililofanyika jana tarehe 17/12/2015 katika ukumbi wa masai club kinondoni jijini dar lilivuta wapenzi na mashabiki lukuki waliovutiwa na kucheza mpaka kuchwee!, mama munira mkazi wa tegeta jijini dar alisema kuwa nimekuja na familia yangu hapa masai club kwa ajili ya kuwashuhudia wakaliwao kwani bendi ni ninayo ipenda sana, namuomba thabit abdul kufanya awezavyo ili burudani tamu kama hizi ziweze kuja na kwetu tegeta.

 

         Show hiyo ambayo ilihudhuliwa na baadhi ya wasanii akiwemo malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa ambae alipanda stejini na kuimba wimbo wake wa "mjini chuo kikuu" huku akishangiliwa kwa nguvu na mashabiki, jambo la kustaajabisha ambalo liliwaacha mashabiki vinywa wazi ni pale mke wa halidy chokoraa cathy chuma alipopanda katika jukwaa la wakaliwao na kuimba wimbo wa taarab "sioni thamani ya pendo" huku akionyesha ujuzi zaidi kwa kupenyeza vipande vyake mwenyewe hali iliyoifanya nyimbo hiyo kupendeza zaidi, zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo zilipigwa katika tamasha hilo:-


CATHERIN CHUMA AKIIMBA WIMBO WA SIONI THAMANI YA PENDO.
KHADIJA OMARY KOPA AKIIMBA WIMBO WA MJINI CHUO KIKUU.
NASRA SHABBAN MUIMBAJI WA WAKALIWAO.
CATHERIN CHUMA AKIIMBA KWA HISIA.
KIBIBI YAHYA MATRON WA WAKALIWAO AKIITIKIA CHORUS.
THABIT ABDUL AKIPAPASA KINANDA.
SUPER BLACK MPIGA SOLO WA WAKALIWAO AKIFANYA YAKE.
DULLAH KINANDA WA WAKALIWAO AKIWAJIBIKA STEJI.
WAMOJA SALUM WA WAKALIWAO NAE ALIKUWEPO
JESCA MTAMU MCHEZA SHOW WA WAKALIWAO AKIWAJIBIKA STEJINI.
AISHA VUVUZELA AKIIMBA KWA MADAHA.
SALHA WA HAMMER Q AKIIMBA KWA HISIA KALI.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni