TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 2 Machi 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAOMBELEZAJI KATIKA KUUAGA MWILI WA KAPTEN KOMBA DAR.

NA KAIS MUSSA KAIS
 
Rais Jakaya Kikwete leo amewaoongoza mamia ya waombolezaji waliofika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuuaga mwili wa mbunge wa Mbinga magharibi Kapt John Komba aliyefariki Jumamosi iliyopita njiani wakati akipelekwa Hospitali ya TMJ.
Mwili wake ulipokelewa kwa heshima huku ukiwa umebebwa na Askari wa bunge.
MUHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIWA NA MKEWE MAMA SALMA WAKITOA HESHIMA ZA MWISHO MBELE YA MWILI WA MAREHEMU KAPTEN JOHN KOMBA.
Ndugu jamaa na marafiki walikuwa katika huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao huyo. Wapo waliopoteza fahamu kutokana na kushindwa kuamini tukio hilo.
Wasanii walimuenzi marehemu Komba kwa kuimba nyimbo za maombolezi ambazo aliziimba enzi za uhai wake wakati wa msiba wa Baba wa Taifa, Hayati J.K.Nyerere mwaka 1998.
Katika salamu zake kwa niaba ya kambi Rasmi ya upinzani Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh.Joshua Nasari ametoa pole kwa familia ya marehemu na taifa.
Mh Nasari alisema kwamba kambi rasmi ya upinzani imeguswa na kifo cha mwanasiasa mwenzao kwani kila mmoja atarejea na huko ndiko kila mmoja atakwenda.
Pia Mh Nasari amesema katika kipindi hiki kigumu ni vyema kila mmoja akasali na kuomba muda wote ili kujiwekea mazingira mazuri huko aendako.
GARI ILIYOBEBA MWILI WA MAREHEMU KAPTEN JOHN KOMBA LIKIINGIA KWENYE VIWANJA VYA KARIMJEE.
Moja ya mambo yaliyohuzunisha ni taarifa aliyoitoa Mh Cyril Chami mbunge wa Moshi vijijini ambapo alisema siku ya Jumamosi ambayo alifariki Mh Komba, aliwasiliana nae kwa simu mda mchache kabla hajazidiwa ambapo Mh Chami alikuwa njiani kwenda kumuona.
JENEZA LILILOBEBA MWILI WA KAPTEN JOHN KOMBA LIKIWEKWA VIZURI TAYARI KWA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO.
Anasema alipofika nyumbani akaambiwa Mh Komba amezidiwa hivyo wamempeleka Hospitali ya TMJ.
MWILI WA MAREHEMU KAPTEN JOHN KOMBA UKIINGIZWA KWA HESHIMA KUBWA NDANI YA VIWANJA VYA KARIMJEE
Mh Chami alienda TMJ hata hivyo alipofika getini alikutana na gari la kubeba wagonjwa likiupeleka mwili wa marehemu Komba chumba cha kuhifadhi maiti.
Kweli binadamu inabidi kuwa tayari muda wote kwani hatujui saa wala dakika ya kurudi kwa muumba wetu. 
Tufanye mambo mema ya kumpendeza Mwenye ez Mungu kwani dunia ni mapito tu.
Mamia wamuaga marehemu John Komba
MASHADA YA MAUA YAKIWA YAMEWEKWA KWA HESHIMA KATIKA JENEZA LA MAREHEMU KAPTEN JOHN KOMBA
Tumuombee safari njema mwenzetu kwani sote tuko njia moja. Amen.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni