TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 21 Julai 2015

KHADIJA OMARY KOPA ATEULIWA KUGOMBEA TUZO AFRICAN MUZIK MAGAZINE AWARD'S NCHINI MAREKANI.

NA KAIS MUSSA KAIS

                  Malkia wa mipasho nchini Tanzania na afika mashariki kwa ujumla Khadija omary kopa ameteuliwa kugombea tuzo za African muzik magazine award's...Afrimma award's za nchini marekani ambazo hufanyika kila mwaka.


      Malkia ameteuliwa kugombea katika kipengele cha "Best female east africa" ambapo hapa anapambana na nyota wengine kutoka africa mashariki kama:-


                                                   1.Aster Aweke wa Ethiopia.

                                                   2.Victoria kimani wa Kenya.

                                                   3.Vanessa Mdee wa Tanzania

                                                   4.Juliana Kanyamozi wa Uganda

                                                   5.STL wa Kenya

                                                   6.Irene Ntale wa Uganda.


       Mashindano hayo ambayo yamekuwa yakijizolea umaarufu kila mwaka yamekuwa yakiwashirikisha wasanii kutoka pande zote za afica kupitia aina tofauti za muziki,. wadau na wapenzi wa mamaa mukubwa khadija omary kopa milango ipo wazi sasa katika kumpigia kura mama yetu ili aweze kushinda, unachotakiwa kufanya ni kuingia katika mtandao na kuandika www.afrimma.com/nominess-2015, hapo utakwenda moja kwa moja katika kipengele cha "Best female east africa" na utaona majina yamepangwa, unachotakiwa kufanya ni kumpigia kura mama yetu malkia khadija omary kopa na hapo tayari utakuwa umemuwezesha kushinda na kuiletea sifa kubwa nchi yetu ya Tanzania na tasnia yetu ya taarab kwa ujumla shime wadau tuanze sasa! naamini kwa pamoja tunaweza!... Mamaa mukubwa is the best!.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni