TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 27 Desemba 2015

HAMISI SLIM:- KWA SASA MARIAM B.S.S NI MUIMBAJI MPYA WA BENDI YANGU YA G5 MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Muimbaji mariam b.s.s. amejiunga rasmi na bendi ya G5 modern taarab akitokea five star's modern taarab zote makazi yao yapo temeke jijini dar es salaam.

MARIAM BSS


         Akizungumza kwa kujiamini mkurugenzi wa G5 hamisi slim alisema kuwa tayari ameshamalizana nae mariam b.s.s. na kwa muda huu ni msanii wa bendi yangu, unajua mariam alikuwa asafiri na wenzake wa five star's modern taarab kwenda mikoani katika sikukuu ya x-mass lakini hawakuelewana na mkurugenzi wake wa zamani Ally J ndipo alipokuja kwangu na tukafanya biashara tukamalizana alisema hamisi slim.


MARIAM BSS AKIWA STEJINI.

       Nae mume wa muimbaji huyo aitwae soda ya kopo alizungumza na mtandao huu na kusema kuwa ni kweli mke wangu amejiunga na G5 modern taarab na tayari ameanza kazi rasmi katika bendi yake hiyo mpya. mtandao huu ulimtafuta Ally J ili athibitishe taarifa hizi za kuondoka kwa muimbaji wake lakini simu yake haikuwa ikipatikana, tunawaahidi kuwaletea maelezo ya Ally J baada ya kuzungumza nae!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni