TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 7 Januari 2016

MZEE YUSUPH:- NIMEAMUA KUMFUKUZA KAZI MUSSA MIPANGO HAPA JAHAZI MODERN TAARAB KWA UTOVU WA NIDHAMU.


NA KAIS MUSSA KAIS.

                 Mkurugenzi wa jahazi modern taarab mzee yusuph leo hii amefunguka kuwa amemfukuza bendi mpigaji wake maarufu wa gitaa la besi mussa mipango kwa utovu wa nidhamu ambao aliuonyesha tokea wanatoka safari ya mombasa na nairobi.

MKURUGENZI WA JAHAZI MODERN TAARAB MZEE YUSUPH AKIWAJIBIKA.

          Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kutwangiwa na mwandishi wa habari hizi, mzee alisema kuwa Mussa amekuwa ni mtu wa nongwa kwa muda mrefu sana na hii ni baada ya kuona kwamba sisi jahazi tunamtegemea sana yeye katika upigaji wa chombo chake, tatizo lilianza wakati wa kurudi ziara yetu ya mombasa na nairobi, matarajio yetu sisi kama viongozi yalifeli hivyo wasanii hawakuwa wamelipwa stahiki zao kama ilivyo ada! ukizingatia kuwa show moja ilivunjika hivyo tukapatana kuwa tutakuja kuwapa pesa zao huku dar baada ya show ya pale mango garden kinondoni,.

           Lakini mussa aliongea maneno mengi sana ya kulaumu na kuona kama anaonewa yeye na wasanii wenzake kitu ambacho sio kweli, alafu cha kushangaza wasanii wenzake hawakuwa wakilalamika kabisa isipokuwa yeye tu!, tulipofika dar na kufanya ile show ya mango wasanii wote tuliwalipa pesa zao akiwemo na huyo mussa ndipo uongozi kwa kauli moja tuliamua kumfukuza kabisa bendi na sio kumsimamisha kama ambavyo inasemekana. kwahiyo kuanzia sasa mimi mzee yusuph nasema kwamba mussa mipango sio msanii wa jahazi modern taarab popote anaweza kwenda kufanya kazi.

MUSSA MIPANGO-MSANII ALIEFUKUZWA KAZI JAHAZI MODERN TAARAB.

         Mtandao huu kwa kutaka kubalansi stori uliamua kumpigia simu mussa mipango na kumuuliza juu ya taarifa hizi za yeye kufukuzwa kazi jahazi, mwanzoni kabisa mwa mahojiano yetu alikili kuwa ni kweli ameondolewa jahazi modern taarab, lakini tulipotaka kujua kwa undani zaidi tatizo haswa ni nini alijibu kwamba yeye hajui ila waulizwe viongozi wa jahazi modern taarab, alipoambiwa kuwa viongozi wa jahazi tayari wao wameshazungumza ya kwao isipokuwa yeye ndio anatakiwa aseme kulikoni? aliamua kukata simu yake...Hilo ndilo sakata la mussa mipango na jahazi modern taarab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni