TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 7 Januari 2016

UONGOZI WA JAHAZI MODERN TAARAB WAONDOA MISHAHARA KWA WASANII WAKE, SASA KULIPWA KWA WIKI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Uongozi wa bendi ya jahazi modern taarab umeondoa kabisa huduma ya kuwalipa mishahara wasanii wake kila mwezi kama ilvyo ada na sasa kulipwa kila mwisho wa wiki.


          Akizungumza haya mkurugenzi wa bendi hiyo mzee yusuph amesema kuwa ameamua kufanya mabadiliko haya baada ya kuona kuwa mambo yamebadilika mno kibiashara na pia kuna baadhi ya wasanii huwa wanafanya kusudi kutokuja kazini wakijua wazi kwamba mwisho wa mwezi kuna mshahara anapata, kwahiyo sasa kila msanii atalipwa kulingana na utendaji wake wa kazi na wala si vinginevyo alisema.


        Akizungumzia mabadiliko haya msanii mmoja mwandamizi wa bendi hiyo ambae aliomba mtandao huu usimtaje jina lake alisema kuwa tayari athari zimeanza kuonekana kwa upande wao kwani madeni yameanza kuwa tatizo ukizingatia show zilizopo ni chache na hata watu ambao wanaingia katika show zao kwa sasa wamepungua sana, tunamuomba mkurugenzi ajaribu kutufikilia haswa sisi wanawake ambao hatuna tunachokitegemea zaidi ya muziki.

WAIMBAJI WA JAHAZI MODERN TAARAB WAKIWA STEJINI.

 

          Mtandao huu unawakumbusha wamiliki wa bendi mbalimbali pamoja na wadau kukutana kwa pamoja na kujadiliana nini cha kufanya ili kuunusuru muziki huu wa taarab nchini kwani kadri siku zinavyosonga mbele hadhi na thamani ya muziki huu imekuwa ikiporomoka kwa kasi ya ajabu.


       

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni