TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 7 Januari 2016

MARUFUKU KWA BENDI YOYOTE KUKOPI NA KUPIGA NYIMBO ZA JAHAZI MODERN TAARAB, ASEMA MZEE YUSUPH.

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Katika kile kinachoonekana sheria za kukopi na kupesti kitu cha mwenzako bila ridhaa yake kuanza kutumika mwaka huu, mkurugenzi wa jahazi modern taarab mzee yusuph leo ametoa kalipio kali kabisa kwa bendi zenye mtindo wa kukopi na kupiga nyimbo za bendi yake pasipo ruhusa yake kwamba atazichukulia hatua kali za kisheria.


MZEE YUSUPH-MKURUGENZI WA JAHAZI MODERN TAARAB.

           Akizungumza kwa hasira na uchungu mkubwa mzee yusuph alisema kuwa watu wamekuwa wakijinufaisha kirahisi rahisi tu kwa kupiga nyimbo za bendi yake katika ma-bar mbalimbali hapa mjini, ila kwa sasa nasema imetosha sitaki na nakataza kuanzia sasa!, bendi yoyote ambayo itakiuka tamko hili basi itakuwa ndio mfano kwa wengine pale nitakapo wachukulia hatua kali za  kisheria na kuwashitaki cosota kwani haki ya nyimbo hizo ninayo mimi, nami ni mwanachama pale cosota pamoja na bendi yangu kwa ujumla.


         Nitakachofanya nitaajili vijana ambao watakuwa wakizunguka katika bar ambazo ni maarufu kwa bendi hizi ndogo ndogo za taarab kufanya show zao humo, na vijana hawa watakuwa na kamera ambazo watazitumia kurekodi bendi hiyo wakati wakiimba nyimbo zetu ili baadae iwe kama ushahidi pale nitakapo waburuza katika mikono ya sheria. wasitegemee kwamba mimi mzee yusuph nitakuja na maskari eneo la tukio la hasha ila vijana wangu watafanya kazi hiyo na kuleta majibu.


         Mtandao huu unapenda kutoa rai kwa bendi zinazohisiwa kufanya hivyo kuacha mara moja kwani kinachokuja tokea hapo baadae ni uhasama baina yao na kuwekeana visasi visivyokwisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni