Jina kaka zema ni maarufu sana nchini kenya hususani katika jiji la nairobi na vitongoji vyake, huyu ni mtangazaji mwenye kipaji kikubwa toka katika redio ya citizen ambae anatangaza kipindi cha taarab kiitwacho rusharoho pamoja na vipindi kadhaa wa kadhaa!.
mtandao huu ulipata bahati ya kufanya mahojiano nae wakati alipotembelea tanzania, ungana nasi ili uweze kumjua vyema yeye ni nani na ametokea wapi mpaka kufikia hapo alipo.
KAKA ZEMA NA MKEWE SIKU YA NDOA YAO. |
KAKA ZEMA:- Mimi ni mkenya nimezaliwa maeneo ya kwale, mimi ni kijana mdogo tofauti na watu wanavyo nifikilia, nimelelewa katika familia maskini, vile vile mimi ni kitindamimba kati ya watoto kumi na moja wa familia yetu na wawili tayari wametangulia mbele ya haki.
UBUYU WA TAARAB:- Vipi kuhusu elimu yako, wapenzi, wadau pamoja na mashabiki zako wangependa kujua zaidi toka kwako.
KAKA ZEMA:- Mimi shule ya msingi nimesomea kule zanzibar, sekondari na chuo kikuu pia nimesoma kule kule zanzibar, vile vile taaluma yangu hii ya utangazaji nimesomea nairobi kenya hivyo naweza kusema kuwa nimelelewa na nchi mbili tofauti yaani kenya na tanzania.
UBUYU WA TAARAB:- Unafikili ni kitu gani haswa kilikupa hamasa na msukumo mkubwa wa wewe kuwa mtangazaji?.
KAKA ZEMA AKIWA STUDIO ZA CITIZEN AKIWAJIBIKA. |
KAKA ZEMA:- Naweza kusema kuwa mimi nimezaliwa na kuwa mtangazaji, nilipokuwa shuleni nilikuwa ni mtu mwenye kelele sana darasani na hata siku nisipokuwepo basi kila mmoja anajua leo zema hayupo, wakati mwingine nilikuwa naigiza kutangaza mpira wa miguu na vipindi vingine.
UBUYU WA TAARAB:- Mpaka sasa upo citizen redio nairobi kenya, je unaweza kukumbuka ni redio ngapi ambazo uwahi kufanyia kazi?.
KAKA ZEMA:- Ni redio kadhaa nimefanyia kazi kama vile redio salaam baada ya hapo nikachukuliwa na bahari fm na hapa bahari nimefanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja ndipo baadae nikajiunga na citizen redio ambayo nipo mpaka sasa.
WATOTO WAWILI WA KAKA ZEMA WAKITABASAMU KWA FURAHA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni