TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 11 Januari 2016

BENDI, VIONGOZI NA WASANII WA TAARAB NCHINI, HAWAPENDI KUANDIKWA WAKIFANYA MAMBO MABAYA KWANINI?.

Na pambe za taarab

              Asalaam aleykum wasomaji wangu wa blog hii bora kabisa ya taarab nchini ya pambe za taarab, tumekutana tena leo hii katika makala hii ambayo inazungumzia udhaifu na uadilifu wa wahusika wa taarab tanzania.

 

                  Leo nitazungumzia hii tabia iliyojengeka miongoni mwa bendi, viongozi na hata wasanii wa taarab nchini tanzania kupinga kuandikwa habari zao pindi wanapofanya mabaya huku wakijua wazi kuwa wao ni kioo cha jamii, viongozi wa taarab ni watu wa ajabu sana, wanapokuwa na habari zao za kuitangaza bendi au albam wanakuwa mstari wa mbele kukutafuta na kukupa ushirikiano wa nguvu ili mradi tu umuandike

 

        Umuhimu wa habari ni kuandika kilicho cha kweli na wala sio kubuni, hata kama habari ikiwa mbaya kiasi gani kinachotakiwa ni kulinda miiko ya uandishi lakini pia ni lazima ubalansi stori kwa kuhoji pande zote mbili ndipo unaweza kuandika habari hiyo, itakuwa maajabu kuona kwamba kila kukicha katika taarab hakuna mabaya yanayotendeka!!, leo hii hata ukiripoti tu msanii flani ameihama bendi flani yenye jina kubwa hapa nchini...viongozi wake wanakujia juu na kusema kuwa eti una mpango wa kuishusha bendi yao jambo ambalo sio kweli.

 

            Huu ni mtandao uliosajiliwa serikalini na kampuni ya brela na kupewa namba "294266" na wala hatufanyi mambo haya kienyeji tu, wasanii mnategemea media kuwatangaza  nasi pia tunawategemea ninyi kupata habari kwahiyo hapo utagundua kuwa sisi ni watu ambao tunategemeana katika kazi zetu, tunachokiomba toka kwenu ni ushirikiano wenu tu na muwe tayari kuandikwa kwa lolote lile ambalo mtandao huu utataka kuripoti. Sote ni binadamu hatujakamilika kwahiyo kukosea ni kawaida kwetu, tujikubali kwahilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni